February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sugu achomoka kwa dhamana, kutinga polisi leo

Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha

Spread the love

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu)-Chadema jana jioni alifanikiwa kupata dhamana baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya asubuhi ya siku hiyo kwa madai ya uchochezi. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Sugu alifika kituoni hapa jana asubuhi akiitikia wito wa jeshi hilo uliomtaka kufanyi hivyo kwa madai ya kukashifu mamlaka za serikali hususani kukejeli ugawaji wa vitambulisho vya mjasiriamali.

Mbunge huyo alipifika kwenye Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu video unayosambaa akionekana ‘kukejeli’ mamlaka za serikali, alizuiwa kutoka.

Sugu anadaiwa kutoa kauli hiyo alipozungumza na wananchi wakati akitoa msaada katika Shule ya Msingi Ikuti, Mbeya. Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani humo lilimpa dhamana majira ya saa 1 jioni baada ya kuwekewa dhamana ya bondi ya Sh 5 milioni. L anatakiwa kwenda kuripoti kituoni hapo.

Urich Matei, Makanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya amesema, kuwa kesi ya Sugu ni ya uchochezi na kwamba, amepewa dhamana huku uchunguzi ukiendela.

error: Content is protected !!