Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yavunja mwiko kwa Mbao FC
Michezo

Yanga yavunja mwiko kwa Mbao FC

Heritier Makambo
Spread the love

BAADA ya kupata ushindi wa mabao 2-1 klabu ya soka ya Yanga kwa mara ya kwanza imefanikiwa kuondoka na pointi 3 mbele ya Mbao Fc, kwenye Uwanja wa Ccm Kirumba, Mwanza. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Toka Mbao Fc ilipopanda daraja katika msimu wa 2016/17 Yanga haikuwahi kupata matokeo kwenye dimba la Ccm kirumba katika michezo mitatu waliocheza ikiwemo na kombe la shirikisho.

Katika michezo sita waliokutana Yanga itakuwa imefanikiwa kuifunga Mbao Fc mara nne, mitatu ikiwa kwenye uwanja wa Taifa na mmoja Ccm Kirumba kwenye michezo ya Ligi Kuu, huku Mbao ikishinda michezo miwili yote wakiwa nyumbani.

Mbao Fc ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ndaki Robert dakika ya (45+2), na kipindi cha pili Heritier Makambo alifanikiwa kusawazisha baoa hilo kwa njia ya kichwa dakika ya (49) na baadae Amis Tambwe akaipatia Yanga bao la ushindi kwa njia ya penati dakika (68)

Yanga bado inaendelea kuwa kileleni kwa pointi 61 baada ya kucheza michezo 25, ikifuatiwa na Azam fc yenye alama 50 baada ya kucheza michezo 24 na Simba nafasi ya tatu ikishika ikiwa na alama 42 baada ya kucheza michezo 17.

Tazama mabao yote hapo chini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!