October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uteuzi wa Rais Magufuli leo hii

Dk. John Magufuli, Rais wa Tanzania

Spread the love

RAIS John Magufuli amemteua Dk. Michael Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).Anaripoti Bupe Mwakiteleko…(endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 20 Februari 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

Taarifa hiyo ya Msigwa inaeleza kuwa, Dk. Ng’umbi amechukua nafasi ya Dk. Fidelice Mafumiko ambaye ameteuliwa kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Ng’umbi alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Jaji Stephen Magoiga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT). Kabla ya uteuzi wa Jaji Magoiga, nafasi hiyo ilikuwa chini ya Jaji Barke Mbaraka Sehel ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

“Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi huo umeanza tarehe 19 Februari 2019,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Msigwa.

error: Content is protected !!