Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu abadili upepo siasa za CCM
Habari za SiasaTangulizi

Lissu abadili upepo siasa za CCM

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

SIASA ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinazidi kuchukua sura mpya baada ya  kujielekeza kwenye  mashambulizi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

CCM imeanza utaratibu wa kumshambulia Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki baada ya kuanza kufanya ziara zake Ulaya na Marekani. 

Akiwa ziarani Kilosa, Morogoro Dk. Bashiri Ally, Katibu Mkuu wa CCM amesema kuwa Lissu ‘hajui shida.’

Dk. Bashiru yupo ziarani Morogoro ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM.

Kwenye ziara hiyo juzi Dk. Bashiru alisema, Lissu anadeka huku akimwomba  Rais John Magufuli amtibu.

“Yupo msomi mmoja anaitwa Tundu Lissu ameugua ugonjwa wa deko, anadeka hajui jembe kwa maisha yake, hajui mpunga unalimwaje wala samaki wanavuliwaje.

“Hajapanda bodaboda muda mrefu na watoto wake hawasomi shule hizi anazunguka dunia nzima kutuchafua.

“Tunao Tundu Lissu wengi Serikalini tumewaamini, tumewapa dhamana ila ukiwatembelea ofisini wanadeka,” alisema Dk. Bashiru.

Alisema, Lissu amekuwa akitembea nchi za Ulaya akisema uonga huku akiamini siku moja atakuwa Rais wa Tanzania.

Akiwa ziarani huko Dk. Bashiru amedai kuwa, Lissu anasumbuliwa na ugonjwa wa kusema uongo, deko, uonevu, dharau, kiburi.

“Namuomba Rais wetu aanze kutibu ugonjwa wa deko. Unasomesha watu wanazunguka kutukana nchi yao na Rais wao?” Alieleza kwa kushangaa.

Wakati mtendaji huo wa juu wa CCM akiyasema hayo, Lissu amekuwa akiendeleaa na ziara yake katika nchi za Ulaya ambapo kwa sasa yupo nchini Marekani akieleza ‘hali ya demokrasia nchini’ na kupigwa kwake risasi.

Kutokana na hali hiyo Dk. Bashiru, alisema kuwa dalili za ugonjwa wa aina ya Tundu Lissu ni kusema uongo, dharau, deko, uonevu, kiburi, majivuno.

Amesema kuwa, manesi na madaktari wa ugonjwa huu ni Watanzania nyie wenyewe.

Amesema kuwa, sehemu ya ugonjwa wa Lissu ni kuota urais wa Tanzania, kuwa na kiburi na kwenda Ulaya kuzungumza lugha za wakoloni.

“Lakini sasa anayemwita dikteta amefuta mashamba kwa ajili ya wanyonge,” amesema.

Hata hivyo amesema, watendaji serikali ambao hawataki kupona ugonjwa Wa na Lissu watafute watafute serikali nyingine.

“Ajira ni hiyari, waandike barua waseme chama hiki hakipendi dhuluma, mimi nadhulumu, hakipendi uongo mimi muongo,” Amesema.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!