Tuesday , 30 May 2023
Home Kitengo Maisha Afya Hospitali ya Benjamini Mkapa kuzindua maabara ya Moyo
Afya

Hospitali ya Benjamini Mkapa kuzindua maabara ya Moyo

Hospitali na Benjamini Mkapa ya Dodoma
Spread the love

HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH), kesho inatarajia kuzindua rasmi maabara ya upasuaji magonjwa ya moyo ikiwemo matundu na kuziba kwa mishipa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza leo tarehe 11, Februari 2019, Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo katika hospitali hiyo, Dk.Wilfred Rutawile alisema wameanza kufanya uchunguzi na kuzibua mishipa ya damu na tayari wagonjwa wawili wamechunguzwa.

“Wagonjwa hawa walikuwa wanasumbuliwa na matatizo ya kifua kwa muda mrefu na wamekuwa wakihudhuria kliniki hapa lakini bado maumivu yalikuwa yakiendelea, tukaamua kuanza kufanya uchunguzi wa mishipa yao ambapo tumefanya,” alisema.

Alibainisha kuwa kwa siku ya jana watawafanyia wagonjwa saba upasuaji huo na wataendelea kutoa huduma hiyo hospitalini hapo.

“Kwasasa tupo na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKIC) kwasababu mashine ni mpya na imekuwepo muda mrefu bila kufanya kazi, kwasababu wao wana uzoefu wamekuja hapa ili kufanikisha kufanyika kwa ufanisi zaidi,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dk. Alphonce Chandika alisema maabara hiyo imeanza kufanya kazi na mashine inayotumika kufanya upasuaji huo imegharimu takribani Sh.5 bilioni.

“Huu mtambo ni wa kisasa na hapa hospitali tayari tuna wataalam watatu, serikali iendelee kuleta wataalam zaidi ili kudumia wananchi, kwa hapa nchini hii ni maabara ya tatu lakini mashine iliyopo hapa ni ya kipekee kwa kuwa una uwezo wa kufanya huduma ya mishipa mingine ya kichwa hata ya miguu,” alisema.

Hata hivyo alisema kuanza kutoa huduma hiyo na huduma mbalimbali za figo kutawezesha kupata wagonjwa kutoka nje ya nchi.

“Tuna mashine ya uvunjaji mawe kwenye figo ambayo ni mashine ya kipekee nchini, tunashukuru sana Rais John Magufuli kwa kuwajali wananchi wake,” alisema.

Naye, Mkurugenzi wa taasisi ya JKCI, Prof. Mohamed Janabi alisema wamefika katika hospitali ya Benjamin kusaidiana na madaktari kutoa huduma hiyo ambayo itawafanya wananchi wasisafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo jiji la Dar es salaam.

“Mgonjwa wa kwanza anatokea Maswa na mgonjwa wa pili anatokea Singida kati yao yupo mgonjwa hakimu, mwanasheria,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema hatua hiyo itapunguza foleni katika taasisi hiyo ambayo kwa mwaka jana iliwafanyia upasuaji zaidi ya wagonjwa 1000.

“Tutapanga utaratibu wa sisi kuwepo hapa ili wataalamu wa hii hospitali wapate utaalam kama wetu ambao tumeanza kutoa huduma hii miaka mitatu iliyopita,” alisema.

Alisema kwa miaka mitatu wamehudumia wagonjwa takribani laki mbili wa magonjwa mbalimbali ya moyo hivyo ni tatizo kubwa.

“Taasisi ya JKCI tunaona wagonjwa kila siku kati ya 250 hadi 300 wa ndani, na tunafanya upasuaji kati ya wagonjwa 8-10 kwa siku, upasuaji wa kusimamisha moyo kati ya mgonjwa mmoja hadi wawili kwa siku,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Madaktari bingwa 10 waliokuwa India warudi na shuhuda nzito kuhusu utalii tiba

Spread the loveMADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo wameendelea kuongezeka katika Taasisi...

Afya

Kipindupindu chabisha hodi Dar, wagonjwa 10 waripotiwa

Spread the love  Ugonjwa wa Kipindupindu umeibuka jijini Dar es salaam ambapo...

Afya

Ujenzi wa zahanati kwa ufadhili wa TASAF wafikia asilimia 95

Spread the love  UJENZI wa mradi wa Zahanati ya Mwanalugali A Kibaha...

Afya

Serikali yatenga Sh. 15 bilioni kukamilisha maboma 300 ya zahanati

Spread the love  SERIKALI imetenga kiasi cha fedha Sh. 15 bilioni, katika...

error: Content is protected !!