October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kuziona Simba, Yanga Sh. 7,000

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu unaowakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo kiingilio cha chini kitakuwa ni Sh. 7,000. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Viingilio vingine katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi 16 Ffebruari, 2019 vitakuwa ni Sh. 30,000 kwa VIP A na 20,000 kwa VIP B na C.

Kuelekea mchezo huo Yanga inatarajia kuweka kambi mkoani Morogoro wakitokea Tanga, huku Simba wakisalia Dar es Salaam ambapo wanajiandaa na mchezo wao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa 12 Februari, 2019.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa kileleni kwenye msimamo wa ligi kwa kukusanya jumla ya pointi 58 baada ya kucheza michezo 23, huku Simba ikiwa kwenye nafasi ya tatu na kukusanya pointi 36 baada ya kucheza michezo 15.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 30 Septemba, 2018 na kumalizika kwa suluhu na kila timu ilifanikiwa kuondoka na alama moja.

error: Content is protected !!