Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Gwajima amfananisha Rais Magufuli na Nabii
Habari za Siasa

Askofu Gwajima amfananisha Rais Magufuli na Nabii

Spread the love

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dk. Josephat Gwajima amemfananisha Rais John Magufuli na Nabii. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akichangia hoja katika mkutano wa wadau wa sekta ya madini uliofanyika leo tarehe 22 Januari 2019 jijini Dar es Salaam, Askofu Gwajima amesema Rais Magufuli amekuwa kama nabii.

“Ahsante sana rais leo umekuwa kama nabii, wakati nimekaa hapa nilisema itawezekanaje nitoke hapa bila kuongea, ingekuwa shida,” amesema Gwajima.

Akichangia kuhusu changamoto zianzoikabili sekta ya madini hapa nchini, Askofu Gwajima ameishauri serikali kuunda timu ya watu wenye uwezo na ushawishi wa kumudu siasa za kibiashara katika kiwango cha kimataifa hasa kwenye kutafuta masoko ya madini nje ya nchi.

“Si kweli hakuna soko la madini, sababu dhahabu yenyewe ni fedha ukiwa nayo ni fedha, isipokuwa tu nilikuwa nashauri, uwe na watu wenye exposure na siasa ya madini, kuunda watu wenye akili na wenye exposure ambao wanaweza kuziikia nchi mbalimbali dunia kutafuta masoko

Kuhusu changamoto ya uwepo wa kodi katika biashara ya madini, Gwajima amesema hashauri kupunguzwa kwa kodi bali serikali iwapunguzie kiwango cha kodi kwa wachimbaji wenye kiwango kidogo cha madini.

“Nilipita Mwadui njiani Maganzo nilishangaa kweli, nikapaki gari watu wakasema huyu Gwajima wakanifuata wakitaka kuniuzia dhahabu, ndani ya saa moja nililetewa bakula la ilog tano limejaa Almasi. Hizi kama zingelipiwa ushuru nchi yetu ingefika mbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!