Monday , 22 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Watoto waishio mazingira magumu waiangukia Serikali
Habari Mchanganyiko

Watoto waishio mazingira magumu waiangukia Serikali

Spread the love

WATOTO wanaolelewa kwenye vituo jijini Dodoma wameiomba serikali kudhibiti taasisi,mashirika na watu binafsi wanaojihusisha na utapeli wa kivuli cha watoto yatima na kujipatia mamilioni ya fedha na misaada mbalimbali ambayo haiwafikii walengwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ombi hilo lilitolewa na watoto wanaolelewa katika kituo cha Shirika la Malezi Endelevu (SHIME) jijini Dodoma Raheli Rafael na Moses Tobias kwa niaba ya wezao wakati walipokuwa wakipokea misaada mbalimbali iliyotolewa na wanavyuo kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Wakizungumza baada ya kupatiwa misaada hiyo iliyotolewa na wanavyuo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) watoto hao wameiomba serikali kupitia wizara husika kuhakikisha wanawadhibiti matapeli ambao wamekuwa na vituo hewa vya kulelea watoto yatima na kujipatia mamilioni na mali.

Raheli Rafael alisema kuwa pamoja na juhudi za makusudi zinazofanywa na serikali kwa ajili ya kuhakikisha watoto yatima wanapata haki sawa kwenye mahitaji yao,bado kuna utapeli unaofanywa  baadhi ya taasisi,mashirika na watu binafsi kwa udanganyifu huo.

“Hivyo sisi kama watoto yatima kwa niaba ya wezetu tunamuomba Rais wetu ambaye yupo mstali wa mbele,kudhibiti vitendo hivyo viovu,kwa kuangalia kwa jicho la upana vituo vya kulelea watoto yatima kutokana na kuwepo kwa udanganyifu wa matapeli,” alisema.

Kwa upande wake Moses Tobias alisema kuwa bado kuna changamoto kwenye vituo vya kulelea watoto kutokana na kuwepo kwa watu binafsi,taasisi na mashirika kuwa na vituo vinavyoishia mifukoni baada ya walengwa.

Alisema wakati watoto hao wakihitajika kusaidiwa katika mahitaji yao ya kimsingi ikiwemo elimu,afya,malazi,mavazi na chakula bado kuna baadhi ya watu wana vituo vyao vipo mifukoni ambao wamekuwa wakijipatia mamilioni ya fedha.

Kwa upande wake mmoja wa wanachuo kitivo cha elimu mwaka wa tatu Ida Theophil alisema kuwa aliiomba serikali kuwekeza kwenye vituo vya watoto yatima ili kuwapunguzia ugumu wa kupatiwa misaada mbalimbali.

Alisema kuwa serikali ikiwekeza kwa kufadhili mahitaji muhimu kwenye hivyo vituo vitaweza kujisimamia wenyewe na pia itatambua kwa wale wanaojihusisha uanzishaji wa vituo visivyosajiliwa kwa mujibu wa kisheria.

Naye Mkurugenzi mkuu wa kituo cha Shirika la Malezi Endelevu (SHIME) Zawadi Mgeni amevishauri vituo vya kulelea watoto yatima vitambuliwe kwa kusajiliwa na serikali kwa lengo la kubaini vinavyojihusisha kuwahujumu watoto hao.

Alisema ili kuondokana na changamoto ya kuwemo na hujuma ya uanzishaji wa vituo hewa serikali ni muhimu ikaviangalia kwa jicho la pili ambalo litakalobaini ubadhilifu na hatimaye misaada ikawafikia walengwa.

Katika hafla hiyo wanavyuo hao walikabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vyakula sabuni, mafuta na vifaa vya elimu kama vile madaftali na sare za shule.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

Habari Mchanganyiko

DCEA yakamata kilo 767.2 za dawa za kulevya, 21 mbaroni

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!