Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hukumu ya Uenyekiti wa Prof. Lipumba Januari mwakani
Habari za SiasaTangulizi

Hukumu ya Uenyekiti wa Prof. Lipumba Januari mwakani

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imehalisha kutoa uamuzi juu ya uhalali wa Msajili wa vyama vya siasa nchini kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Shauri hilo namba 13 la Mwaka 2016 lilipangwa kutolewa uamuzi tarehe 30 Novemba, 2018, lakini lilikwama baada ya Jaji Dk. Benhajj Masoud kutokuwepo mahamani hapo.

Imeelezwa kuwa Jaji Masoud yumo kwenye usikilizaji wa kesi za jinai nje ya Dar es Salaam.

Uamuzi huo umepangwa kutolewa tarehe 15 Januari Mwaka 2019.

Prof. Lipumba alitangaza kujiuzulu uenyekiti wa CUF, tarehe 6 Agosti 2015. Akarejeshwa kwenye nafasi yake na Jaji Mutungi, tarehe 13 Juni 2016.

Prof. Lipumba aliondoka ndani ya CUF katikati ya kipindi cha kampeni kwa madai kuwa haungi mkono makubaliano yaliyofikiwa na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ya kukakaribishwa Edward Lowasa, kuwa mgombea wao wa urais.

Lowassa, waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri, alijiengua CCM kati kati ya mwaka 2015.

Alitangaza kujiunga na Chadema siku tatu baada ya kuenguliwa katika mbio za urais.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!