Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Upelelezi wa Vigogo wa Almasi haujakamilika
Habari Mchanganyiko

Upelelezi wa Vigogo wa Almasi haujakamilika

Spread the love
ARCHARD Kalugendo, mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort) na Edward Rweyemamu, mthamini wa madini ya almasi wa Serikali wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Washtakiwa hao wamefikisha mwaka mmoja na miezi mitatu rumande ikielezwa kuwa upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika.

Kalugendo na Rweyemamu walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Septemba 15, 2017 kujibu shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Dola1,118,291.43 za Marekani (zaidi ya Sh. 2.4 bilioni).

Leo Desemba 3, 2018 wakili wa Serikali, Elia Athanas amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Athanas amedai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Washtakiwa hao wanatetewa wa wakili Nehemiah Nkoko na leo hakuwepo mahakama hapo wakati kesi hiyo inatajwa.

Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka aliwahoji washtakiwa alipo wakili wao na kujibiwa kuwa hawana taarifa zake.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Mashauri aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 17, 2018.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabiliwa na shtaka la kuisababishia Serikali hasara ya Sh. 2.4 bilioni.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa Serikali na waajiriwa wa Wizara ya Madini na Nishati, waliisababishia Serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!