Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Michezo Nahodha wa Madrid amkataa Conte
Michezo

Nahodha wa Madrid amkataa Conte

Spread the love

NAHODHA wa Real Madrid, Sergio Ramos anaonekana kutokukubaliana na ujio wa kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ndani ya kikosi hicho baada ya kutimuliwa Julen Lopetegui kufuatia kuwa na matokeo mabaya kwenye michezo ya ligi kuu nchini humo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Nahodha huyo anaonekana kutofurahishwa na aina ya uwendeshaji timu wa Conte, kutokana na kuingia mara kwa mara kwenye migogoro na wachezaji. 

Hali hiyo inakuja baada ya Conte kuwa katika moja ya makocha wanaopendekezwa kwenda kuchukua mikoba ya Lopetegui ambaye alitimuliwa jana baada ya kupoteza mchezo kwa bao 5-1 dhidi ya Barcelona siku ya Jumapili na timu hiyo kwa sasa ipo chini ya Santiago Solar kwa muda.

Conte ambaye alitimuliwa kwenye klabu ya Chelsea mwisho wa msimu uliopita baada ya kuwa katika matatizo na baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo akiwemo Eden Hazard ambaye huwenda akahamia Madrid katika majira ya joto.

Kwenda kwake Madrid huwenda kukakwamisha uhamisho Hazard kutoka Chelsea kutokana ya kutokuwa na maelewano mazuri baina ya wawili hao hapo awali.

Matatizo hayo binafsi kati ya Conte na baadhi ya wachezaji wa Chelsea yalipelekea timu hiyo kushika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi na hivyo kushindwa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katika msimu huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

error: Content is protected !!