Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ushirikiano ndiyo silaha pekee itakayowalinda waandishi-MCT
Habari Mchanganyiko

Ushirikiano ndiyo silaha pekee itakayowalinda waandishi-MCT

Kajubi Mkajanga, Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Spread the love
KAJUBI Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), amesema silaha pekee itakayowakwamua waandishi wa habari nchini katika mazingira ya magumu wanayopitia ni kuongeza ushirikiano katika utendaji wa kazi zao za kila siku na kuongeza ufanisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo leo tarehe 4 Oktoba, 2018 visiwani Zanzibar katika mkutano maalumu wa wanachama wa MCT wenye lengo la kujadili ufinyu wa vyombo vya habari katika kufanya kazi na jamii.

Kajubi amesema waandishi wengi wa Tanzania wamekuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu ya ufanyaji kazi zao licha ya tasnia ya habari kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kila siku.

Amesema mazingira magumu ya ufanyaji kazi kwa waandishi yamakuwa yakiongeza kila siku licha ya tasnia hiyo kutumika kwa kiwango kikubwa katika harakati za maendeleo ya jamii husika.

Owino Opondo, mwezeshaji katika mkutano huo, amesema kumekuwepo na mazingira ya kupigwa na kudhalilishwa kwa waandishi wa habari bila ya wahusika wanaofanya hayo kuchukuliwa hatua hali iliyojenga hofu kwa waandishi wanapofanya kazi zao.

“Kumekuwepo kwa matukio mengi dhidi ya waandishi na vyombo vyao, ikiwemo kufungwa vyombo vya habari, kutishwa, kuteshwa kwa waandishi, lakini hadi sasa hakuna wahusika waliohusika na vitendo hivyo waliokamatwa,” amesema Opondo.

Mbali hayo Opondo amesisitiza uwepo na weledi kwa waandishi wa habari kwani fani ya habari ni fani kama zilivyo fani nyingine zinazohitaji weledi katika utendaji wake wa kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

error: Content is protected !!