
Kajubi Mkajanga, Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Spread the love
Kajubi Mkajanga, Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Kajubi amesema waandishi wengi wa Tanzania wamekuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu ya ufanyaji kazi zao licha ya tasnia ya habari kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kila siku.
Amesema mazingira magumu ya ufanyaji kazi kwa waandishi yamakuwa yakiongeza kila siku licha ya tasnia hiyo kutumika kwa kiwango kikubwa katika harakati za maendeleo ya jamii husika.
Owino Opondo, mwezeshaji katika mkutano huo, amesema kumekuwepo na mazingira ya kupigwa na kudhalilishwa kwa waandishi wa habari bila ya wahusika wanaofanya hayo kuchukuliwa hatua hali iliyojenga hofu kwa waandishi wanapofanya kazi zao.
“Kumekuwepo kwa matukio mengi dhidi ya waandishi na vyombo vyao, ikiwemo kufungwa vyombo vya habari, kutishwa, kuteshwa kwa waandishi, lakini hadi sasa hakuna wahusika waliohusika na vitendo hivyo waliokamatwa,” amesema Opondo.
Mbali hayo Opondo amesisitiza uwepo na weledi kwa waandishi wa habari kwani fani ya habari ni fani kama zilivyo fani nyingine zinazohitaji weledi katika utendaji wake wa kazi.
More Stories
Takukuru yavimbia wakandarasi, ‘yarejesha’ mil 420 Tanesco
IGP Sirro: Hatufungui kesi za madai, migogoro ya ardhi
Panyabuku waanza kubaini TB