Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Michezo Yanga yamchongea Kotei TFF
Michezo

Yanga yamchongea Kotei TFF

Spread the love

MARA baada kiungo wa Simba, James Kotei kumpiga ngumi ya mgongo mlinzi wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael wakati wakiwania mpira kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliowakutanisha mahasimu hao wikiendi iliyopita uongozi wa Yanga waibuka na kulaani kitendo hicho ambacho kimeonekana siyo cha kiungwana. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Klabu hiyo imekwenda mbali zaidi kiasi cha kuiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusu vitendo ambavyo si vya kiungwana vilivyotokea kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa suluhu uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo, Dismas Ten alisema yapo matukio kadhaa yaliyojitokeza kwenye mchezo huo yalikuwa siyo ya kiungwana ambayo kila mwanamichezo hawezi kuvumiliana.

“Sisi kama klabu tumeshaandika barua kwenda kwenye mamlaka husika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa vitendo hivyo na nina amini hatua stahiki zitachukuliwa kutokana na bodi ya ligi wako imara kusimamia taratibu zinazoongoza mpira wetu,” alisema Dismas Ten.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!