March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jengo la Benjamin Mkapa lawaka moto

Spread the love

MOTO umezuka katika jengo la Benjamin Mkapa Tower lililopo maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam katika ghorofa ya nne hali iliyosababisha kuzua taharuki kwa watu waliokuwa katika jengo hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Muda mchache baadan ya kutokea kwa moto huo ambao chanzo chake bado hakijafahamika, Kikosi cha Jeshi la Zimamoto kimefanikiwa kuuzima moto ambao madhara yake bado hayajafahamika.

Moto huo ambao umesababisha watu kukimbia huku na huko, inadaiwa baadhi wamekwama katika moja ya lifti katika jengo hilo.

 

error: Content is protected !!