Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watanzania milioni 21 hawapati maji safi na salama
Habari Mchanganyiko

Watanzania milioni 21 hawapati maji safi na salama

Ukosefu wa maji safi
Spread the love

KUKOSEKANA kwa usimamizi bora wa rasilimali za maji kumetajwa kuwa sababu ya watanzania takribani milioni 21 kutofikiwa na huduma ya maji safi na salama. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamebainishwa jana tarehe 3 Oktoba 2018 na wadau walioshirikia katika hafla ya utoaji tuzo kwa waandishi mahiri wa habari za maji iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Shahidi wa Maji, Mhandisi Herbert Kashililah alisema kuwa, uhaba wa fedha na uwajibikaji katika rasilimali za maji ni moja ya sababu ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi. Ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia (WB) ya mwaka 2017 inaeleza kuwa takribani watanzania milioni 21 hawafikiwi na huduma hiyo.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji mada katika hafla hiyo, William Mwaluvanda ambaye ni mtaalam wa masuala ya rasilimali za maji, alisema licha ya Tanzania kuwa na rasilimali za maji ikiwemo maziwa makubwa matatu, mabonde 9 ambayo 7 kati yao hutumiwa na nchi jirani, lakini rasilimali hizo zimeshindwa kuwasaidia watanzania ipasavyo.

Mwaluvanda alieleza kuwa, kukosekana kwa usimamizi mzuri wa rasilimali hizo ndiyo chanzo cha baadhi ya wananchi hasa wa vijijini kukosa huduma ya maji safi na salama.

Kufuatia changamoto hiyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso alisema serikali itanedelea kuongeza bajeti kwenye sekta ya maji ili kufanikisha malengo yake ya kwamba ifikapo mwaka 2020 asilimia 85 ya watanzania wawe wamefikiwa na huduma ya maji safi na salama.

Hata hivyo, Aweso alitoa wito kwa sekta binafsi kujitokeza katika kuwekeza kwenye sekta ya maji hasa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kutoka katika rasilimali za maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!