Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: Fedha za kurudia uchaguzi zikatibie wazee
Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Fedha za kurudia uchaguzi zikatibie wazee

Spread the love

BARAZA la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limetaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kubadilisha utaratibu wa kuwapata wabunge, katikati ya Bunge. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Roderick Lutembeka amesema, fedha nyingi zinatumika kwenye uchaguzi, bila sababu za msingi.

Amesema, “tunaweza kuokoa mamilioni ya shilingi zinazotumika kwenye chaguzi za marudio, ikiwa tutabadilisha utaratibu wa kuwapata wabunge, katikati ya kipindi cha Bunge.”

Kwa mujibu wa Lutembeka, NEC inaweza kubadilisha utaratibu kwa kuruhusu chama ambacho mbunge wake amejiuzulu au kufariki dunia, kuteuwa mtu mwingine kushika nafasi hiyo.

“Fedha hizi zinazotumika katika chaguzi za marudio, zinapotea bure. Sisi katika Chadema, tunapendekeza zitumike kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa wazee. Tunataka ziboreshe maisha yao, badala ya umalaya wa kisiasa,” ameeleza.

Amesema, wazee nchini wanakabiliwa na matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma bora za afya, madawa na wataalamu maalum wa magonjwa ya wazee.

Anasema, “…utoaji wa huduma za afya kwa wazee hauridhishi. Kuna ukosefu wa dawa na wataalamu waliojikita kuhusu masuala ya wazee. Lakini serikali inapoteza fedha katika chaguzi ambazo zinaweza kuepukika.”

Kauli ya Lutembeka inakuja katika kipindi ambacho lundo la wabunge na madiwani wa upinzani, wanavihama vyao vyao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika hatua nyingine, baraza hilo limeitaka serikali kutunga sheria ya wazee itakayoipa meno sera ya wazee katika utekelezaji wake, ikiwemo kuondoa changamoto zinazokabili kundi hilo.

Vile vile, limeitaka serikali kutoa mafao ya uzeeni kwa wazee wote waliotumika taifa kupitia serikalini au sekta binafsi.

Naye mwenyekiti wa baraza hilo, Hashim Juma Issa, ameishauri serikali kuunda chombo maalum kitakachoshughulikia matatizo ya wazee.

Amesema, “hii nchi ni kubwa sana na wazee wako wengi hivyo siyo rahisi kwa serikali kuwafikia wote, iwapo Chadema ikishika dola itaanzisha chombo cha kushughulikia changamoto za wazee.

Vile vile, inatakiwa kuwepo viti maalum kwa ajili ya wazee ili kundi hilo lipate wawakilishi wa kusemea changamoto zao bungeni.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!