Saturday , 13 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba, Yanga yaingiza Sh 404 mil
Michezo

Simba, Yanga yaingiza Sh 404 mil

Spread the love

Mchezo wa Ligi Tanzania bara namba 72, uliowakutanisha mabingwa watetezi Simba dhidi ya Yanga jana 30 septemba, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam umeingia Sh. 404,549,000 baada ya kuingiza watazamaji 50,168. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kwenye mgawanyo wa mapato hayo waliokuwa wenyeji wa mchezo huo klabu ya Simba wamepata kiasi cha Sh. 194,962,105, Bodi ya Ligi wamepata Sh. 29,244,315, gharama za mchezo ni Sh. 22,745,578, huku Baraza la Michezo lilipata Sh. 3,249,368  na Chama cha Mpira wa Miguu Dar es Salaam kiliambulia Sh. 9,748,105.

Lakini pia ghalama ya kodi ya ongezeko la thamani iliokwenda mamlaka ya mapatao Tanzania TRA ni Sh. 61,710,864.41 ambayo ni asilimia 18 ya fedha iliyopatikana huku wakala waliokuwa wakikatisha tiketi hizo za kieletroniki Selcom wao walipata Sh. 17,901,293.25.

Ikumbukwe mchezo huo uliisha kwa sare ya bila kufungana na hivyo kila timu kuambulia alama moja na kuendelea kubakia katika nafasi zao zilezile kwenye msimamo wa ligi kuu, Simba ikishika nafasi ya tano ikiwa na alama 10, huku Yanga ikisalia kwenye nafasi ya pili na kubakia na alama zao 12.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Usiku wa Ulaya kinawak tena leo

Spread the love  LIGI ya mabingwa barani ulaya itaendelea tena leo ambapo...

Michezo

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni Usiku wa Kisasi

Spread the love  LEO utarejea ule usiku pendwa kabisa kwa mashabiki wa...

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

MichezoTangulizi

Samia aipa tano Yanga

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga licha ya...

error: Content is protected !!