Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Oil yaokoa maisha ya Mhandisi kivuko cha MV Nyerere
Habari MchanganyikoTangulizi

Oil yaokoa maisha ya Mhandisi kivuko cha MV Nyerere

Spread the love

OIL imetajwa kuwa miongoni mwa sababu zilizookoa maisha ya Mhandisi wa Kivuko cha MV Nyerere, Alphonce Charahani, aliyeokolewa akiwa hai baada ya kupita saa 48 tangu kivuko hicho kizame katika Ziwa Viktoria. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wakizungumza baada ya kumuokoa mhandisi huyo, asubuhi ya leo tarehe 22 Septemba 2018, baadhi ya waokoaji walisema mbinu ya Mhandisi Charahani ya kujipaka oil mwilini, ilimsaidia kuzuia maji ya ziwa hilo kuingia kwenye vinyweleo vyake.

Kivuko hicho kilizama kwenye ajali iliyotokea tarehe 20 Septemba 2018 wakati kikisafirisha abiria kutoka kisiwa cha Bugorora kwenda Kisiwa cha Ukara kwenye Ziwa Victoria.

Baada ya kuokolewa, Mhandisi Charahani alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Busya kilichopo kisiwani Ukerewe kwa matibabu zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!