Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Michezo Rais CAF aguswa na ajali ya MV Nyerere
Michezo

Rais CAF aguswa na ajali ya MV Nyerere

Spread the love

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi msiba wa waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi kati ya Ukara na Bugorara, Ukerewe. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Rais wa CAF, Ndugu Ahmad ametoa pole kwa Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli na watanzania kiujumla na pia ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huo mzito uliosababisha majonzi makubwa kwa Watanzania.

“Naungana na Watanzania na Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa msiba huo mzito kwa Tanzania,” alisema Rais wa CAF.

Wakati huohuo, Karia kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa waliofariki katika ajali hiyo.

Karia amesema ni huzuni kubwa kwa Taifa na Watanzania kwa ajali hiyo iliyopoteza wapendwa wetu.

Amesema ajali hiyo imepoteza wana familia ya Mpira wa miguu ambao walikuwa wakifuafilia ama mashabiki wa mchezo huo lakini pia ajali hiyo imepoteza nguvu kazi ya Taifa.

TFF inaungana na Ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kupoteza wapendwa wao. Pia inawapa pole na kuwatakia afya njema majeruhi waliookolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo Uingereza, Uholanzi zote kukupa pesa

Spread the love Siku ya leo EURO 2024 kupigwa katika viwanja mbalimbali,...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

error: Content is protected !!