March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Falsafa ya Askofu Bagonza kuzama kwa MV Nyerere

Spread the love

ANAANDIKA Baba Askofu Dk. Benson Bagonza (PHD), Daktari wa Falsafa na Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.

MAPENZI YA MUNGU NA MAPENZI YETU

Siyo kila kifo ni mapenzi ya Mungu, hata kama Mungu anajua kila kifo. Sio kila ajali ni mapenzi ya Mungu hata kama Mungu anajua kila ajali, tukumbuke pia alimuacha mwana wake kuuawa hata kama alikuwa na uwezo wa kuzuia, alimwacha mwana wake kusalitiwa hata kama alikuwa na uwezo wa kumkomesha usaliti wake.

Hatua zote za maendelea zina ukurasa wa majanga, Dreamliner na Bombadier usiote janga lake, SGR janga lake ni kiama, Stiggler’s Gorge ina janga la kuangamiza mamilioni kwa siku moja kingo za bwawa zikipasuka, meli mpya ya abiria 2,000 ni kaburi la halaiki linaloelea majini.

Uwezo wetu upimwe kwa kushughulikia majanga si kwa kuchochea majanga, poleni wafiwa, ugueni pole majeruhi, tufarijiane watanzania.

error: Content is protected !!