Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Standard Chartered yatoa Bil 1.5 kuchenga reli
Habari za Siasa

Standard Chartered yatoa Bil 1.5 kuchenga reli

Spread the love

TANZANIA kupata mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46 sawa na zaidi ya shilingi trilioni 3.3 kutoka kwa Benki ya Standard Chartered Group kwa ajili ya kujenga kipande cha Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kuanzia Morogoro hadi Makutupora, mkoani Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yameelezwa na Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Bill Winters Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Jijini Dar es Salaam.

“Tunajenga Reli hiyo ya Kisasa kutoka Dar es Salaam – Morogoro hadi Makutupora ambazo ni awamu mbili lakini pia tutajenga reli hiyo kuelekea Isaka mpaka Mwanza na baadaye Rusumo ambapo wenzetu wa nchi ya Rwanda, tutasaidiana, wao watajenga reli hiyo kutoka Rusumo hadi Kigali” Aliongeza Dk. Mpango.

Dkt. Mpango ameishukuru Benki hiyo kwa kukubali kugharamia ujenzi wa Reli hiyo ya kisasa ambayo lengo lake ni kuimarisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo kwenda bara na nchi jirani za Maziwa Makuu na zile ambazo hazipakani na Bahari.

Naye Bill Winters, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Group, ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa kiuchumi na kwamba Benki yake itatoa mkopo huo na kuahidi kuwa balozi wa kuelezea mafanikio makubwa ya kiuchumi ya Tanzania kwa wadau wengine.

Katika kikao hicho, Bw. Bill Winters aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo nchini Kenya na nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki Bw. Lamin Manjang na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo nchini Tanzania Bw. Sanjay Rughani, ambapo pia Benki hiyo inafanya shughuli zake hapa nchini kwa kipindi cha miaka 101 sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!