Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Michezo Mo Salah aiwekea masharti Misri ili aitumikie timu ya Taifa
Michezo

Mo Salah aiwekea masharti Misri ili aitumikie timu ya Taifa

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa Livepool na timu ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah amekipa masharti Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) ambayo wakishindwa kuyatimiza atajiuzulu kuitimukia timu yake ya Taifa. Anaripoti Halidi Mhina … (endelea).

Salah kupitia Mwanasheria wake, Abbas Issa ameiandikia barua EFA kuitaka kuwadhibiti mashabiki wa timu hiyo, wasimsumbue nyota huyo pindi anapokuwa katika kambi ya timu yake ya Taifa nchini humo.

Mwanasheria huyo amesema Salah analazimika kujiuzulu kuitumikia timu yake ya taifa kutokana na kero anazozipata kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo, katika maeneo tofauti tofauti anapokuwa nchini Misri.

Katika barua hiyo, mwanasheria huyo amekitaka EFA vurugu kutoka kwa mashabiki hao ambazo Salah anazipata ikiwa ni pamoja na mashabiki wa soka kumgongea chumbani kwake hotelini usiku wa manane wakitaka kupiga picha naye na watashindwa kutekeleza hilo, mteja wake atajiuzuru kuitumikia timu yake ya Taifa.

Mambo yaliyoainishwa kwenye barua hiyo iliyotumwa tarehe 23 Agosti, 2018, imekitaka EFA wakemee vitendo vya mashabiki kuweka kambi nje ya chumba cha hoteli cha Salah, wasimgongee usiku kutaka kupiga naye picha, wasimzonge akiwa mazoezini.

Sahal anatakiwa kuwa na walinzi wawili kila anapokuwa na wakati akiwa hotelini wawe nje ya chumba chake, simu zote zinazopigwa kuelekea chumbani kwake zizuiliwe, hatafanya matangazo, mahojiano, mikutano, matukio ya wadhamini, ziara rasmi kwa niaba ya EFA na kuchukuliwa uwanja wa ndege na kumpeleka moja kwa moja hotelini kwa hadhi ya kipekee.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

Michezo

Meridianbet inakwambia beti mechi spesho za EURO sasa

Spread the love Wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet wamekuja na Spesho ODDS...

error: Content is protected !!