Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sababu za kukamatwa Zitto hizi hapa
Habari za SiasaTangulizi

Sababu za kukamatwa Zitto hizi hapa

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

JESHI la Polisi linaendelea kumshikiria Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa mahojiano kwa kosa ya kutoa kauli za uchochezi katika mkutano wa hadhara alioufanya Kata ya Kijichi, Temeke, anaandika Faki Sosi.

Zitto alikamatwa mapema leo asubuhi nyumbani kwake na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Chang’ombe kwa mahojiano kwa makosa hayo ambayo anadaiwa kufanya katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani wa kata ya Kijichi.

Kwa mujibu wa viongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto anahojiwa kwa kutoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani kwa wananchi na kujenga chuki kwa serikali yao.

Maneno hayo yaliyopelekea Zitto kushikiliwa na kuhojiwa ni pamoja na kusema: “Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.”

Zitto pia anadaiwa kusema: “Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.”

Timu ya mawakili wa chama cha ACT-Wazalendo na ndugu na jamaa wa Zitto wapo pamoja naye katika mahojiano hayo na wataendelea kutoa taarifa kila kinachoendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

error: Content is protected !!