Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa JPM atangaza vita na wakuu wa mikoa
Habari za Siasa

JPM atangaza vita na wakuu wa mikoa

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli ametangaza vita na wakuu wa mikoa watakaoshindwa kuweka mikakati na mipango ya kujenga viwanda katika maeneo yao ili kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Serikali ya viwanda,” anaandika Moses Mseti.

Amesema mkuu wa mkoa yeyote atakayeshindwa kujenga viwanda katika mkoa wake hatasita kumuondoa kwenye nafasi yake kwa kuwa atakuwa tayari ameonesha hana uwezo wa kuchapa kazi ili kuendana na kasi yake katika usimamizi wa rasilimali za Taifa.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwatex, Nyakato Ilemela na kuhudhuliwa na wananachi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza.

Amesema katika ziara zake za kikazi atakapokuwa anapita katika mkoa wowote ule na kukuta hakuna kiwanda anachokizundua, mkuu wa mkoa husika hatasita kumuondoa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

“RC (mkuu wa mkoa) kama leo napita, kesho kutwa napita lakini hakuna viwanda, huyo lazima aondoke na lengo la serikali ni kukusanya kodi na kutengeneza ajira kwa vijana wetu, wengine unapita hakuna kiwanda,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema mkuu wa mkoa atakayeshindwa kuanzisha viwanda vingi katika maeneo yao hata endelea kufanya nao kazi kutokana na serikali kupambana kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara hivyo kama hakutakuwepo na viwanda ukusanyaji wa kodi na uchumi wa Taifa utashuka.

Pia Rais Magufuli amesema katika miaka ya awali mkoa kama Mwanza ulikuwa na viwanda vya kutosha lakini wazee waliokuwa wakivisimamia viwanda hivyo wameviua na kwamba wanapaswa kujiuliza na kujitafakali.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba na Meya wa Jiji hilo, James Bwire kuacha marumbano na mgogoro wao uliodumu kwa kipindi cha takribani miezi sita kwa kuwa wao ni chama kimoja.

Amesema kuwa wao wanapaswa kushikamana kwa ajili ya manufaa ya watanzania na kwamba baada ya miaka mitano ni lazima watowe hesabu yao kwa wananchi na kwamba wote ni watumishi wa watanzania wote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!