
Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo
KIONGOZI wa Chama Cha ACT-Wazalendo ameachiwa kwa dhamana alipokuwa anahojiwa katika kituo cha Polisi cha Chang’ombe kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi, kabla ya kukamatwa tena sasa kwa makosa ya kutoa takwimu, anaandika Faki Sosi.
Zitto ambaye alikamatwa mapema asubuhi na kupelekwa katika kituo cha Chang’ombe kwa mahojiano, lakini alipoachiwa kwa dhamana alikamatwa tena na polisi na kupelekwa katika kituo cha polisi Kamata, Kariakoo kwa mahojiano ya takwimu alizozitoa wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itakadi na Uenezi wa cha hicho, Ado Shaibu amesema kuwa chama Zitto amehojiwa na Polisi kwa kutuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kwenye kampeni za udiwani Kata ya Kijichi, Temeke.
Shaibu amesema kiongozi wao aliachiwa majira ya saa sita kwenye kituo hicho na kukamatwa tena na kupelekwa kwenye kikosi maalumu cha Kamata.
Mawakili waliomsindikiza Zitto kwenye mahojiano hayo ni pamoja na Steven Mwakibolwa na Venas Msebo ambao wamefuatana naye tena katika kituo cha polisi Kamata.
Kwenye kituo cha Polisi cha Chang’ombe Zitto amedhaminiwa na wadhamini wawili kwa sharti la kurudi tena kituoni hapo Jumatatu.
More Stories
Mrithi wa Maalim Seif, siri nzito
Rais Magufuli amuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya
Dk. Bashiru: Nilipata taarifa za uteuzi mitandaoni