Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Matokeo ya darasa la 7 haya hapa, shule za serikali hoi
Elimu

Matokeo ya darasa la 7 haya hapa, shule za serikali hoi

Spread the love

BARAZA la Mitihani Taifa NECTA limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2017, na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa 2.4% ukilinganisha na ule wa mwaka jana 2016, anaandika Faki Sosi.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa wa NECTA Dk. Charles Msonde, na kusema kuwa watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 na zaidi, kati ya alama 250 ambazo walitakiwa kupata.

Dk.. Msonde amesema kwamba kati ya waliofaulu wasichana ni 341, 020 ambayo ni sawa na 70.93% na wavulana ni 321, 015, ambao ni sawa na 74.80%, na idadi ya watahiniwa wote waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76%.

Katibu Mkuu huyo amesema kwamba ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kingereza na Hisabati umepanda kati ya 4.25% na 10.05% ukilinganisha na mwaka jana, huku masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii ukishuka kati ya 3.56% na 13.97%.

Sambamba na matokeo hayo pia Dk. Msonde amezitaja shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo
St. Peters – Kagera, St, Severine – Kagera, Alliance ya Mwanza, Sir. John – Tanga, Palikas – Shinyanga, Mwanga – Kagera
Hazina – Dar es salaam, St. Anne Marie – Dar es Salaam, Rweikiza – Kagera na Martin Luther – Dodoma.

Dk. Msonde amezitaja shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa ambazo ni Nyahaa – Singida, Bosha – Tanga, Ntalasha – Tabora, Kishangazi – Tanga, Mntamba – Singida, Ikolo – Singida, Kamwala – Songwe, Kibutuka – Lindi, Mkulumanzi – Tanga, Kitwai A – Manyara.

KUJUA MATOKEO YOTE INGIA HAPA

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

error: Content is protected !!