Tuesday , 18 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Daktari wa Kanumba afunguka mazito kesi ya Lulu
Habari MchanganyikoMichezoTangulizi

Daktari wa Kanumba afunguka mazito kesi ya Lulu

Lulu Michael (kulia)
Spread the love

MAHAKAMA ya Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa jamhuri kwenye kesi inayomkabili msanii wa filamu, Elizabeth Michael (Lulu), anayedaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia ambapo daktari wake na ofisa upelelezi wametoa, ushahidi, anaandika Faki Sosi.

Leo mbele ya Jaji Sam Rumanyika, aliyekuwa daktari familia ya Kanumba Dk. Paplas Kagaiga ametoa ushahidi.

Wakili wa Serikali, Batilda Mushi alimuongoza daktari huyo kutoa ushihidi ambapo amemtaka aseme alichoshuhudia akiwa kama daktari wa familia.

Dk. Kagaiga amedai kuwa Aprili 7 mwaka 2012, saa 6 usiku akiwa kwenye kituo chake ya tiba St Anne alipigiwa simu na mdogo wake Kanumba, Sethi Bosco akimwambia kwamba nyumbani kwao kuna tatizo.

Dk. Kigaiga amedai kuwa alifuatwa na Bosco ofisini kwake na kwenda wote nyumbani na walipofika walimkuta Kanumba amedondoka chini.

Baada ya kuona hali aliyokuwa nayo Kanumba aliamua kumpima sukari na shinikizo la damu (presha) ambapo alibaini sukari ipo chini na mapigo ya moyo yalikuwa hayapigi.

Dk. Kagaiga alimuomba Bosco amvalishe Kanumba nguo kwa alimkuta akiwa na taulo ili wampeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Amedai kuwa alipofika Muhimbili kitengo cha dharura Kanumba alipimwa na kuonekana amefariki.
Wakili Mushi: Unamfahamu Elizabeth Micheal (Lulu)?

Shahidi: Ndiyo

Wakili Mushi: Unamfahamu kivipi?.

Shahidi: Namfahamu kupitia marehemu Kanumba.

Wakili Mushi: alikuwa kama nani

Shahidi: Namfahamu kuwa alikuwa mpenzi wa marehemu Kanumba.

Wakili Mushi: Siku ya tarehe 7 Aprili ulimuona Lulu wakati gani

Shahidi: Saa 11 alfajiri

Wakili Mushi: Ulimuona wapi?

Shahidi: Bamaga Sinza.

Shahidi huyo alieleza kuwa alimpigia simu (Lulu) akiwa Oysterbay polisi ambapo polisi walimuomba awasiliane na Lulu ili wamtie mbaroni ambapo baadaye alienda nao hadi Bamaga alipokuwawepo Lulu na kumkamata na kuondoka naye.

Baada ya kumaliza maelezo hayo wakili wa utetezi, Peter Kibatala alianza kumuuliza maswali shahidi huyo kutokana na ushahidi ulioutoa mahakamani hapo.
Kibatala: Shahidi umesema kuwa una Advance Diploma (Astashahada ) ya masuala ya afya , nitakuwa sahihi nikisema kuwa wewe ni Clinical Officer.

Shahidi: Sio Sahihi

Kibatala: Wewe mtu mwenye Degree (Shahada) waaitwa (MD)nani yupo juu kitaaluma.

Shahidi: Yupo juu mwenye Shahada (Md)

Kibatala: Umewahi kumfanyia Uchunguzi Kanumba wa uvimbe kichwani

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kwanini ulipofika Nyumbani kwa Kanumba ulianza kumpima Sukari?.

Shahidi: Mara nyingi mtu anapodondoka Sukari inashuka.

Kibatala: Ulimkuta Kanumba yupo chini uliwahi kufahamu ni nani aliyemuweka Kanumba chini?.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ulipofika chumbani kwa Kanumba uliona shuka za kitanda zimevugika.

Shahidi: Sikuwahi kuzingatia mazingira

Kibatala: Ni kweli kwamba chumbani kulikuwa kuna chupa ya Pombe.

Shahidi: Sikuwahi kuona

Kibatala: Unafahamu (Brain Oedema)

Shahidi: Uvimbe wa kichwa

Kibatala: Unasababishwa na nini?

Shahidi: Inategemea

Kibatala: inaweza kusababishwa kupooza (stroke)

Shahidi: Ndio

Kibatala: inaweza kusababishwa na Hasira ambayo inaweza kupelekea mishipa kupasuka.

Shahidi: Haiwezekani

Kibatala: Mtu akiwa amekunywa pombe na anahasira anaweza kupata mstuko wa moyo( heart attack)

Shahidi: Ndiyo.

Kibatala: Ni sahihi kwamba Mshtakiwa alikuwa akipiga simu mara kwa mara kujua hali ya afya Kanumba.

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi kwamba kwamba wakati Lulu anakupigia Simu alikuwa anafikiri kuwa Kanumba amezimia

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Ni sahihi kwamba Lulu alikuwa anawasisi kuwa wewe ulikuwa unampigaia simu ili umkutanishe na kanumba amabaye alikuwa ana ogopa kwa sababu ya wivu mkali wa kanumba

Shahidi: Siyo sahihi

Kibatala: Kwanini Mshtakiwa alikubali kukutana na wewe ilhali ulisema alikuwa anahofia kuonana na wewe, ulitumia njia gani kumshawishi?.

Shahidi: Yeye alinipigia simu kuniuliza kuwa Kanumba amefariki na kutaka tuonane Bamaga.

Baada ya maswali hayo wazee wa Baraza wa Mahakama hiyo nao wameuuliza maswali kwa shahidi pamoja na kutaka kujua kama Kanumba alipata maumivu yoyote.

Mzee wa Baraza namba moja: Ulipofika chumbani kwa Kanumba pale alipodondoka alikuwa amevaa vazi gani?

Shahidi: Taulo.

Mzee wa Baraza namba mbili: Unaweza kugundua kuwa mtu aliyedondoka kama ametumia Pombe?

Shahidi: Hapana, mpaka umfanyie vipimo.

Mzee wa Baraza namba mbili: ulimfanyia vipimo kanumba?

Shahidi: Ndio sukari na Presha.

Mzee wa Baraza namba tatu: Uligundua maumivu mengene kwenye mwili wa Kanumba.

Shahidi: Hapana.

Wakati huo huo Jamhuri ilimleta shahidi mwingine, Easter Zafania ambaye ni ofisa mpelelezi aliyekuwa akifanya kazi kwenye ofisi ya mkuu wa upelelezi mkoa wa Kinondoni.

Wakili wa Serikali, Yusuph Abudi alimuongoza shahidi kutoa ushahidi wake na kusema tarehe 7 Aprili mwaka 2012 alipokea simu ya maagizo kutoka kwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Kinondoni, aende Sinza nyumbani kwa Kanumba.

Shahidi huyo aliieleza mahakama kuwa alipata maagizo hayo majira ya saa 9 usiku na aliongozana na askari pamoja na wasanii wa filamu wanane mmoja wao akiwa ni Ray Kigosi hadi nyumbani kwa Kanumba na alipofika alibaini kuwa kwenye nyumba hiyo kuna ishara ya msiba kutokana na watu kujaa.

Ameeleza kuwa baada ya kujitambulisha alipokelewa na ndugu yake Kanumba, Sethi Bosco aliyekwenda kumuonyesha chumba cha Kanumba ambapo aliingia na askari watatu.

Shahidi huyo alieleza kuwa alipoingia kwenye chumba hicho aliona kitanda kikiwa kimevugika, pembeni aliona meza yenye chupa ya soda aina ya Sprite pamoja na chupa kubwa ya Wisky na grasi.

Shahidi huyo amedai kuwa alishuhudi michirizi ya rangi nyeusi kwenye ukuta iliyochirizika mara mbili na baadaye alimpigia simu afande wambura ambaye alimtuma na kumpa taarifa alichokiona.

Easter amedai kuwa alipofika Osyerbay alikuta daktari wa Kanumba, Kagaiga ambaye walimtumia kumkamata Lulu na kumkabidhi kwa mkuu wa upepelezi.

Baada ya kumaliza maelezo hayo, Kibatala aalimuuliza kama anakumbuka alimpeleka Lulu hospitali na alikuwa anasumbuliwa na nini

Shahidi: Sikuweza kujua.

Kibatala: Ni sahahi kwamba ulipokuwa unampeleka Lulu Hospitali uliongozana na mama yake.

Shahidi: Sikumbuki.

Kibatala: Ni Sahihi Lulu alikuwa na Maumivu mapajani kutokana na mapanga aliyopigwa na Kanumba.

Shahidi: Sijui.
Kibatala: Hukuwahi kuchukua maelezo ya Daktari kuhusu ugonjwa wa Lulu kutokana nawewe ndiye uliyekuwa ukisimamia upepelezi wa kesi yake

Shahidi: Haikuwa kazi yangu.
Baada ya Kibatala kumaliza wazee wa Baraza nao walipata nafasi ya kuumuliza shahidi pamoja na kutaka kujua kuhusu maumivu ya Lulu.

Mzee wa Baraza namba moja: Ndani ya Chumba cha Kanumba kulikuwa na hali yoyote ya vurugu?

Shahidi: Siwezi Kuthibitisha.

Mzee wa Baraza namba mbili: Ulipoenda kufanya upelelezi pale kwenye ukuta uliosema umeona rangi nyeusi hukuona kitu kingene kimeganda?

Shahidi: Hapana

Mzee wa Baraza namba tatu: Baada ya kumkamata Lulu alikulalamikian ana maumivu kweli au sio kweli?

Shahidi : Hakuwahi kulalamika maumivu.

Mzee wa Baraza namba tatu: Hospitali ulienda naye kufanya nini?

Shahidi: Hospitali nilimpeleka kutokana na yeye kulalamika maumivu kwa mkuu wa upelelezi.

Kesi hiyo itaendelea Oktoba 23 mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

CoRI: Waandishi wa habari 16,000 hawana mikataba ya ajira Tz

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

error: Content is protected !!