Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wakili Kibatala afunguka sakata la Tundu Lissu
Habari za SiasaTangulizi

Wakili Kibatala afunguka sakata la Tundu Lissu

Peter Kibatala (kushoto) akiwa na Tundu Lissu
Spread the love

BAADA ya tukio la kijinga, la kitoto, lisilo na mantiki wala lisilojenga heshima yoyote kwa washambuliaji; la kushambuliwa kwa risasi Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania (Tanganyika) Tundu Lissu, baadhi yetu tuliamua kukaa kimya kwanza ili kutoa nafasi kwa tafakari (reflection) kuchukua nafasi yake kwa kuwa tukio lile lina implications kubwa sana kwetu.

Tafakari imekwisha na tuko tayari kwa safari bila kujali nini kimemtokea rafiki yetu, kaka yetu, rais wetu wa TLS, mteja wetu na partner wetu katika mapambano mbalimbali.

Tulitoa pia nafasi kwa vyombo husika kuonesha umahiri na umakini wake; si tu ndani (intrisically) bali hata kwa muonekano hata kwa wale wasiobobea katika uchunguzi (efficiency not only being practiced, but being seen to be practised).

Tumefanya kazi mara kadhaa na jeshi la polisi katika shughuli za kuwawakilisha wateja mbalimbali, akiwemo Tundu Lissu; na maoni yetu kuhusu Jeshi hilo tunaya-reserve kwa sasa.

Hayo yote si ya muhimu sana, lakini la muhimu na lililotuibua ni kauli kadhaa za hivi karibuni kuhusiana na kile kinatajwa kuwa ni ushahidi wa muhimu ambao anao (anaweza) kuwa nao dereva wa Lissu ambaye ametajwa kwa majina kadhaa (Simon, Adam na hata “dereva wa Lissu”).

Kwanza, sisi ni Mawakili si tu wa Lissu, bali hata wa dereva huyo. kinachotushangaza ni namna ambavyo suala lake linakuwa handled kiasi kwamba kama si tu ile general feeling iliyonayo umma kwamba driver yule ni shujaa kwa kile kidogo alichofanya kuokoa maisha ya Tundu Lissu, basi pengine angekuwa tayari amehukumiwa katika Mahakama ya Public Opinion kwamba pengine kwa namna fulani anahusika na tukio lile.

Pamoja na kwamba conclusion za iwapo anahusika au la ni za kichunguzi, lakini jeshi la polisi lina wajibu wa kutunza heshima, faragha na hadhi ya dereva yule isipokuwa tu pale linapokuwa na uhakika kwamba pengine kuna namna mbaya ambayo amehusika katika tukio lile; vinginevyo inakuwa kama inaletwa innuendo inayoweza kumuathiri si tu yeye, bali hata familia yake kwani Lissu anapendwa; Na anapendwa kweli hapa Tanzania.

Kama kuna watu walikuwa hawalifahamu hili, sasa wanafahamu pasi na shaka yoyote. Kama kuna mtu anabisha; basi afanye jitihada za kufanikisha kuruhusu maombi ya wazi kwa Tundu Lissu bila kizuizi.

Polisi wanasema wanamtafuta/linamuhitaji, dereva yule kupitia vyombo vya habari na sina uhakika kama limechukua hatua yoyote ya kisheria chini ya Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Cap 20, RE 2002) kumfahamisha rasmi yeye au Mawakili wake (nikiwemo Mimi) au ndugu zake au hata basi wanachama wenzake rasmi kwa maandishi kwamba anahitajika kwa mazungumzo/mahojiano.

Sheria haizungumzii polisin kuanza kutangaza kupitia vyombo vya habari kumhitaji shahidi; na hata pale mahitaji yanapoelekeza kwamba njia hiyo itumike, mahitaji ya katiba yetu yanaelekeza kwamba njia hiyo inatumika kwa namna inayomtunza muhusika.

Majuzi tu tulisikia Jeshi hilo likidai kwamba Lissu hakufikisha rasmi taarifa ya yeye kuwa hatarini na badala yake alienda kulalamika kwenye vyombo vya habari na kwamba Jeshi lisingeweza kushughulikia taarifa za namna hiyo; leo hii nalo linasema linamtufa dereva wa Lissu kwa sababu za kiuchunguzi kwa namna hiyo hiyo waliyosema haifai kufanyia kazi.

Jeshi la Polisi linafahamu dereva yupo Nairobi, Kenya akipatiwa matibabu ya kisaikolojia na kama katika zama hizi za leo kuna mtu (we na au asiwe na madaraka makubwa na uzoefu wa kutosha) ambaye hafahamu kwamba Post Traumatic Stress Disorder huwa si lazima ionekane usoni kwa muathirika, bado tuna safari ndefu sana, sana. Kwa hakika, wataalamu wa haya mambo ya psychology na mental trauma wanafahamu kwamba hata ile tu mtu aliyepitia a a very stessful experience kama ile kuwa na furaha usoni kinyume na matarajio ya wengi; nayo ni alama ya PTSD, na ni hitaji la matibabu na uangalizi wa karibu.

Logic nyingine ya kichunguzi inaelekeza kwamba Tundu Lissu pia kwa kuwa yu hai, bila shaka anafahamu na aliona kilichotokea; vipi yeye umuhimu wa maelezo yake? Hawezi kuhojiwa sasa kwa kuwa bado ni mgonjwa (kimwili na kisaikolojia pengine), si sawa?

Tuseme basi, for the sake of the argument, dereva si psychologically mgonjwa na obviously jeshi linafahamu hayupo nchini kwa sasa; ipi rahisi kati ya kutafuta njia mbadala za kumuhoji kwa njia za kisasa ambazo zinatambuliwa na sheria ya ushahidi (Cap 67, RE 2002) na maamuzi ya Mahakama za Rufani ya hivi karibuni kutoka huko alipo, na kuendelea kusubirisha hicho kipande cha upelelezi kinachomsubiri dereva huyo mpaka siku atakaporudi; na huku wananchi wakisubiri namna jeshi la polisi linavyoshughulikia suala hili nyeti?

Mambo haya ndiyo yanatufanya tuzidi kusisitiza uchunguzi huru wa kutoka nje ya nchi ili pengine tuongeze tija na crediblity katika si tu suala la shambulio la Lissu, bali hata mengine kama ya kupotea kwa Ben SaaNane pamoja na matukio mengine ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi, na yale ambayo wananchi wana shauku kubwa kufahamu hatima zake kiuchunguzi.

1 Comment

  • Mimi nilidhani ndio mfumo kisheria wa kutumia waandishi / vyombo vya habari! Maana nasikia oh Lissu alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba anafuatwa na watu, oh Lema, Bulaya, Halima Mdee, Nassari, n.k wanatishiwa kuuwawa, oh madiwani wa CHADEMA wamehongwa ili watoke kwenye chama!
    Kama sio mfumo rasmi wa kisheria, basi nanyi wanasheria mjitafakari. Kumbuka unapomnyoshea mtu kidole vingine hushangaa na kukukumbusha na wewe!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

error: Content is protected !!