Monday , 22 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Trump atembeza bakuli
Kimataifa

Rais Trump atembeza bakuli

Spread the love

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameomba ufadhili kwa ajili ya ujenzi wa ukuta ili kusaidia kuwafukuza wahamiaji kutoka nchini Mexico.

Mwezi uliopita alifuta mpango wa rais wa zamani wa Marekani Barack Obama uliofahamika kama “Dreamer” ambao ulikuwa unawalinda wahamiaji 690,000.

Hata hivyo, wanademokrat wenye ushawishi katika Bunge wamekataa mapendekezo hayo mapya.

Rais Trump aliliambia Bunge la Congress lililo na wabunge wengi kutoka chama cha Republican wengi kuwa lina miezi sita kukubaliana kuhusu sheria ya kuwasaidia Dreamers.

Hawa ni vijana ambao walipelekwa nchini Marekani kinyume cha sheria kama watoto na hivyo wanakabiliwa na hatua ya kufuzwa kutoka nchini humo.

Chini ya sera za Obama, vijana hao walikuwa na uwezo wa kuomba vibali vya kufanya kazi na kusoma, lakini wakosoaji wanasema kuwa mpango huo ni sawa na kuwapa kinga wahamiaji haramu.

Tangu mpango huo uanze kutekelekwa karibu hali ya wahamiaji 100,000 imebadilika kati ya karibu wahamiaji 690,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!