Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dawa za nguvu za kiume zateka Bunge
Habari Mchanganyiko

Dawa za nguvu za kiume zateka Bunge

Jengo la Bunge la Tanzania mjini Dodoma
Spread the love

MBUNGE wa Konde,Khatibu Haji (CUF) amedai kuwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume limekuwa likiwasumbua Watanzania wengi na kuihoji serikali kama kuna hatua inachukua ili kukabiliana na tatizo hilo, anaandika Dany Tibason.

Akiuliza swali la nyongeza leo bungeni,Haji alidai kuwa tatizo hilo pia limekuwa likiwasumbua baadhi ya Wabunge kwani wamempelekea waraka (memo) wakieleza shida zao juu ya tatizo hilo.

“Mheshimiwa Spika hapa katika meza yangu nina ‘memo’ chungu nzima kutoka kwa waheshimiwa wabunge akiwemo Rashid Shangazi, Joseph Selasini, wote wakielezea shida ya jambo hili,” amesema

“Mheshimiwa Spika hivi sasa kuna utitiri wa matangazo ya biashara ya dawa za kuongeza nguvu za kiume kuna matangazo mengi yanatolewa na kusambaa nchini, jambo ambalo linaashiria ukubwa wa jambo hilo.

“Je Wizara inachukua hatua gani zinazochukuliwa kuhusu utumiaji wa dawa kiholela.

“Mheshimiwa Naibu Spika tendo la raha linahitaji furaha kuna taasisi imeeleza kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi 10 duniani ambayo wananchi wake wamepoteza furaha.

“Sasa ni miaka 50 ya uhuru, je Serikali kwanini nchi yetu iko katika nafasi ya 10 mwisho duniani kwa kupoteza furaha mmekosea wapi,? alihoji Mbunge huyo.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Dk.Hamisi Kigwangala alikiri Watanzania wengi kusumbuliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!