February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Pigo lingine kwa Manji, avuliwa Udiwani

Yusuf Manji

Spread the love

YUSUF Manji, diwani wa CCM katika Kata ya Mbagara, amevuliwa udiwani kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila sababu za msingi, anaandika Mwandishi Wetu.

Taarifa zinasema, Manji amevuliwa wadhifa huo kufuatia kukaidi kuhudhuria vikao hivyo.

Kwa sasa, Manji yuko mahabusu ya Segerea akituhumiwa kwa makosa mbalimbali, yakiwamo kutumia madawa ya kulevya na kukutwa na sare za jeshi.

Taarifa zinasema, Manji alipoteza sifa ya kuwa diwani kabla ya kukamatwa. Tangu kuwa diwani amehudhuria kikao kimoja tu.

error: Content is protected !!