Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Moto waua wanafunzi 7 Kenya
Habari Mchanganyiko

Moto waua wanafunzi 7 Kenya

Spread the love

WANAFUNZI saba katika shule ya sekondari ya wasichana (Moi Girls High School) iliyopo Kibera, katika mji wa Nairobi nchini Kenya wamepoteza maisha baada ya moto kuzuka katika bweni, anaandika Hamisi Mguta.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu nchini humo, Fred Matiang’i ambaye alitembelea shule hiyo baada ya kutokea kwa tukio hilo, amesema leo mapema asubuhi  wanafunzi 10 waliojeruhiwa wamefikishwa katika hospitali ya Taifa ya Kenyatta.

Taarifa kutoka kwa Mkuu wa kituo cha Polisi wa Kibera, Enos Maloba imeeleza kuwa wanafunzi hao 10  walikuwa wakisumbuliwa na kushindwa kupumua kutokana na moshi uliotokana na moto huo lakini waliwahishwa hospitali.

Maloba amesema anaamini chanzo cha moto huo kimetokana na hitilafu ya umeme na kuongeza kuwa timu ya uchunguzi bado inaendelea kutafuta chanzo.

Hata hivyo, Matiang’i  amesema “Rais Uhuru Kenyatta ametuma wachunguzi kujua tatizo na kuwasilisha ripoti ya uchunguzi huo mwishoni mwa Semptemba 2, mwaka huu”.

Baadhi ya wazazi waliofika katika shule hiyo kutazama hali za watoto wao

Matiang’i amesema kuwa shule hiyo imefungwa kwa wiki mbili wakati uchunguzi ukiendelea na kuwa  wanafunzi wa kidato cha nne wataendelea na masomo yao ifikiapo siku ya Ijumaa na watasaidiwa kuendelea na masomo yao wakati ambapo wanajianda kufanya mtihani wa kidato cha nne wa KCSE.

Hata hivyo wazazi wamejitokeza kwa wingi kwenda kuchukuwa watoto zao baada ya mkuu wa shule hiyo kuwatangazia kuwachukua watoto hao.

Bwana Matiang’i aliandamana na gavana wa Nairobi Mike Sonko.

Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini humo mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliotibiwa baada ya kisa hicho alisema kuwa moto huo ulianza saa saba usiku.

Alisema kuwa bweni lililochomeka lilikuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza na kwamba kulikuwa na makelele ya wanafunzi waliojaribu kujinusuru mbalii na mkanyagano huku wasichana wakijaribu kutoka ndani ya bweni hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!