Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yafukuza wafanyakazi 2744
Habari Mchanganyiko

Serikali yafukuza wafanyakazi 2744

George Simbachawene, Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Spread the love

SAKATA la kuwasaka wafanyakazi wa serikali wenye vyeti feki limeacha kilio kwa wanachama 2744 wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Nchini (TALGWU), anaandika Moses Mseti.

Kutokana na hali hiyo wanachama hao wameondolewa katika ajira zao kati ya wanachama 93,000 wa TALGWU kwa nchi nzima.

Hayo yamebainishwa katika mkutano wa nusu mwaka wa wenyeviti wa mikoa wa chama hicho, waliokutana jijini Mwanza, katika kikao cha kikatiba cha kutathmini mwenendo wake kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kuelekea kwenye mkutano mkuu wa chama hicho.

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Rashid Mtima, amesema chama hicho kumepitia kipindi kigumu na kwamba wataendelea kukusanya taarifa za wanachama wao wanaohusika na sakata la kutofikia elimu ya sekondari kwa sasa.

Mtima amesema kwamba ipo haja ya kutafuta tafsiri ya kisheria ya namna mambo yalivyofanyika kwa serikali kuwaondoa watumishi hao serikalini bila kuzungumza na chama chao.

“Wanachama wetu wanaolipwa na fedha za halmashauri wengi hawapati mishahara kwa wakati nah hii siyo halali kabisa kwa sababu katika halmashauri zingine makato ya mifuko ya jamii yanalimbikizwa hayapelekwi kabisa. Kwahiyo tunaiomba serikali iangalie mshahara wa wtumishi ulipwe na serikali kuu kwa ngazi zote,” amesema Mtima.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, amesema shirikisho hilo linaendelea kufanya majadiliano na serikali namna ya kuwalipa stahiki zao watumishi walioondolewa kazini na kuzishughulikia rufaa zilizowasilishwa na watumishi hao.

“Hatuko nyuma tunaendelea kupigania maslahi ya wafanyakazi na naamini yote yatapatiwa ufuimbuzi hivi karibuni kwasababu wiki hii tutakutana na makatibu wakuu wa wizara ya kazi na ajira.

“Matatizo ya watumishi tutayatatua, kwa wale wa darasa la saba wengine tayari wamerudishwa kazini, masaibu yanayoendelea kuwakumba watumishi wasio na makosa tutapambana nayo,” amesema Nyamhokya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari Mchanganyiko

Prof. Mbarawa aanika mafanikio ya TMA

Spread the loveSHUGHULI za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zimeimarika...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!