WAANGALIZI wa uchaguzi wa nje ya nchi ya Kenya wakiongozwa na Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, wamepinga yaliyosemwa na mgombea urais kupitia muungano wa NASA, Raila Odinga kuwa uchaguzi haukuwa wa haki, anaandika Irene Emmanuel.
Waangalizi hao wa Jumuiya ya Madola wamesema hayo baada ya kuibika kwa malalamiko yaliyotolewa na Odinga kupitia muungano wa NASA kuwa kumekuwa na udanganganyifu kwenye uhesabuji wa kura kwani fomu 34A haikujumlishwa.
“…Uchaguzi ulikuawa huru na haki, NASA na Jubilee wasubiri Tume imalize kazi ya kujumlisha matokeo hayo.” amesema Thabo Mbeki.
Leo ni siku ya tatu tangu uchaguzi ufanyike huku zikiwa zimebaki siku nne kabla ya matokeo rasmi kutolewa.
Leave a comment