Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wachimbaji wadogo Sikonge wamwaga fedha serikalini  
Habari Mchanganyiko

Wachimbaji wadogo Sikonge wamwaga fedha serikalini  

Wachimbaji madini wadogo wadogo
Spread the love

KIKUNDI  cha wachimbaji wadogo kinachomiliki mgodi wa dhahabu wa Kapumpa uliopo tarafa ya Kitunda wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora kimeongoza kwa kulipa mrabaha (royalty) wa zaidi ya Sh. 30 milioni serikalini kwa kipindi cha miezi mitatu kati ya migodi 617 yenye leseni, anaandika Mwandishi Wetu.

Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi wa Madini  wa Kanda hiyo,  Salim  Salim, kwa niaba ya Kamishna wa madini nchini, Benjamin Mchwampaka, katika taarifa yake  juu ya uchimbaji mdogo wa madini katika kanda hiyo, alisema leseni ya kikundi cha wachimbaji wadogo wa mgodi wa dhahabu wa Kapumpa  imeongoza kwa kulipa  Sh. 30.42 milioni kwa kipindi cha kati ya Mei na Julai, mwaka huu.

Aidha, leseni ya umoja wa wachimbaji wadogo wa dhahabu ya  wilayani Nzega Mkoa wa Tabora imefuatia kwa kulipa mrabaha wa Sh. 24.5 milioni, huku kikundi cha madini cha Tumaini kikishika nafasi ya tatu kwa kulipa Sh 22.4 milioni .

“Leseni ya mgodi wa Shukrani Chacha Chacha  wa Wilayani  Sikonge umeshika nafasi ya nne kwa kulipa mrabaha wa Sh. 14.9 milioni na mgodi wa Gregory Kibusi Gallid uliopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wenyewe umelipa Sh.  3.99 milioni,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!