Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Mongella atoa neno kwa wakazi wa Mwanza
Habari Mchanganyiko

Mongella atoa neno kwa wakazi wa Mwanza

John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Spread the love

WANANCHI mkoani Mwanza wametakiwa kupenda kushiriki kikamilifu katika kupima Afya na kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka na wanayofanyia kazi ili kuweza kuondokana adha za kukumbwa na magonjwa yanayoweza kuepukika, anaadika Mwandishi Wetu.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa huo, John Mongella wakati akipongeza kamati ya ulinzi na usalama ya mkoani hapo pamoja na viongozi mbalimbali kwa kufanya usafi katika eneo la Soko la Kiloleli lililopo Manispaa ya Ilemela.

“Sisi vingozi na watumishi wa Umma ndio tuwe mstari wa mbele kupima afya na kuzingatia usafi wa mazingira ili kuweza kuwahamasisha wananchi ambao wamekuwa wakiogopa kupima afya zao kwa kuhofia kukutwa na mangonjwa makubwa, kitu ambacho kinahatarisha maisha ya wanajamii wengi.

Aidha, Mongella aliutaka uongozi wa soko la Kiloleli kugawa meza za wafanyabiashara zilizoachwa wazi kwa watu wanaohitaji ili kuweka mazingira katika hali ya usafi.

Naye mkuu wa vikosi vya Jeshi la Wananchi mkoa wa Mwanza, Kanali Albert Kitumbo alisema maadhimisho hayo yanaadhimishwa kwa kuwahamasisha wananchi kufanya usafi na kupima afya ili waweze kuishi kwa amani na kuzijenga familia nyingi.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo la Kiloleli ambalo maadhimisho siku ya Mashujaa kimkoa yalifanyika hapo, wamewataka wananchi wengine kupenda kujitokeza kushiriki kwenye shughuli za kijamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!