Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Buchosa yakabiliwa na uhaba wa watumishi, vifaa
Habari Mchanganyiko

Buchosa yakabiliwa na uhaba wa watumishi, vifaa

Halmashauri ya wilaya ya Buchosa
Spread the love

HALMASHAURI ya Buchosa Wilaya ya Sengerema, Mwanza, inakabiliwa na upungufu wa vifaa vya ofisi, vifaa vya uchoraji ramani na vifaa vya kutayarisha hati pamoja na kabineti za kuhifadhia ramani kitendo ambacho kinasababisha utendaji duni katika idara ya ardhi, anaandika Moses Mseti.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Crispin Luanda, wakati akitoa taarifa fupi ya utendaji kazi wa idara ya ardhi kwa Angelina Mabula, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, anayendelea na ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani hapa.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa halmashauri hiyo ina vifaa duni vya upimaji ardhi ikiwemo darubini ya kizamani ya T2 na kuitaka serikali kuisadia vifaa vya kisasa ili kuleta utendaji kazi wenye tija kwa watumishi wa idara hiyo.

“Idara ya ardhi Buchosa ina watumishi wa ardhi wa kada mbalimbali, sisi halmashauri tunauhitaji wa afisa ardhi wawili, Afisa mipango miji wawili, mthamini wawili na wapima ardhi wasaidizi wane lakini waliopo ni wawili,” amesema Luanda.

Luanda amesema tatizo ukosefu wa mfumo wa ukusanyaji wa kodi za ardhi umesababisha , lengo lao la kukusanya kodi ya ardhi kiasi cha Sh. 5,000,000 na kusababisha wakusanye kiasi cha Sh. 2,113,486 sawa na asilimia 42 katika mwaka wa fedha wa 206/17.

Kwa upande wake Mabula amesema kuwa pamoja na halmashauri hiyo kukabiliwa na tatizo la vifaa na watumishi, lakini amebaini kuna mapungufu ya utunzaji kumbukumbu ya mafaili kutokana na ukosefu wa masjala.

Amesema kuwa, licha ya halmashauri hiyo ilioanzishwa Novemba, 2015 kuomba watumishi, waliopo ni wazembe kutokana na mafaili ya viwanja kutunzwa hovyo kitendo ambacho alihofia kinaweza kusababisha baadhi ya mafaili kuibiwa.

“Nyaraka ya ardhi (viwanja) kweli inatunziwa mezani, mtu akichukua faili akaondoka nalo si itakuwa imepotea,? kweli faili zinakaa mezani kwa mtu mkurugenzi (Crispin Luanda) fanyieni kazi hilo suala,” amesema Mabula.

Emmanuel Kipole, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, amesema ukosefu wa baraza la ardhi la wilaya hiyo, unasababisha wananchi wilayani humo wenye migogoro ya ardhi kusafiri umbali mrefu kwenda mkoani Geita kutafuta usuruhishi baada ya kutoka ngazi za vijiji na kata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!