Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya Manji yapigwa kalenda
Habari Mchanganyiko

Kesi ya Manji yapigwa kalenda

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeahirisha kesi inayomkabili Yusuph Manji, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, anaandika Hamisi Mguta.

Manji ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu hapa nchini anakabiliwa na kesi ya kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na mihuri kadhaa ya jeshi hilo kinyume cha sheria.

Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa leo, haikusikilizwa kutokana na mahakama kuambiwa kwamba upelelezi wake haujakamilika.

Aidha, jana mtuhumiwa huyo alikwama kufika mahakamani hapo kwa madai kwamba ni mgonjwa na anadaiwa kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Madai hayo ya Manji kuumwa yametolewa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na wakili wake.

Kesi ya mfanyabiashara huyo imepangwa kusikilizwa Agost 4, mwaka huu.

Manji alisomewa mashtaka saba Julai 5 mwaka huu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na watuhumiwa wenzake, kwa makosa ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!