Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Masaibu’ ya wanawake wagonga kokoto Mbeya
Habari Mchanganyiko

‘Masaibu’ ya wanawake wagonga kokoto Mbeya

Machimbo ya kokoto
Spread the love

WANAWAKE wanaojishughulisha na uchimbaji kokoto katika kijiji cha Kibaoni kata ya Chokaa Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya wameelezea adha wanazokumbana nazo katika kazi zao katika jitihada za kujikwamua kiuchumi, anaandika Esther Macha.

Wamesema wanalazimika kufanya kazi hiyo ngumu na katika mazingira magumu kutokana na hali duni za kimaisha katika familia zao na kwamba wangeweza kufanya shughuli zingine lakini hawana mitaji ya kuanzisha biashara ndogondogo ili kukidhi mahitaji ya familia.

“Pamoja na juhudi kubwa kuchimba na kuponda kokoto lakini tunaziuza kwa Sh. 1,000/= kwa ndoo ya plastiki. Hatuna vitendea kazi na vifaa vya usalama kwani vifaa hivyo ni gharama na hatuna fedha za kununulia,” amesema Clementine Justin mmoja kati ya wanawake wanaochimba kokoto.

Elizabeth Emmanuel, mwanamama mwingine amesema kuwa kwa wastani wachimabji wa kokoto katika eneo hilo hupata kiasi cha Sh. 3,000/= ambayo haikidhi mahitaji ya kuzihudumia familia zao.

“Soko la mauzo ya kokoto limekuwa changamoto kwetu kwani kuna siku huwa tunakosa kabisa wanunuzi wa kokoto, licha ya kuwepo wajenzi wengi katika wilaya ya Chunya,” amesema Elizabeth.

Samwel Komba, Diwani wa Kata ya Chokaa, amesema ni vyema wanawake hao wajiunge katika vikundi ili wapate mikopo mbalimbali inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwani kata hiyo imepata mikopo yenye thamani ya Sh. 80 milioni.

Sophia Kumbuli, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Chunya amesema wananchi wote wenye nia ya kuhijusisha na ujasiriamali katika wilaya hiyo wanaweza kujiunga katika vikundi vidogo viodogo ili wapewe mikopo.

“Wilaya ya Chunya inaongoza mkoani Mbeya kwa kutoa mikopo kwa wingi kwa wanawake na vijana. Wananchi wabuni miradi ya maendeleo na wapate mikopo, wafanye biashara halali ili walipe kodi itakayoboresha huduma za jamii kama shule, barabara na zahanati,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!