August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Urais wa TFF ‘patachimbika’

Jamal Malinzi, Rais wa TFF

Spread the love

MBIO za kuwania nafasi Urais wa Shirikisho la Mpira Miguu Tanzania (TFF), zinazidi kushika kasi ambapo watu mashuhuri katika medani hiyo wanaendelea kujitokeza, anaandika Shafiyu Kyagulani.

Ally Mayai Tembele, mchambuzi maarufu wa mpira wa miguu hapa nchini ambaye pia amewahi kuwa nahodha wa Klabu ya Yanga mwanzoni mwa naye amejitosa katika kinyang’anyiro cha nafasi ya urais wa TFF akifanya jumla ya waliochukua fomu kufikia nane.

Wengine waliochukua fomu mpaka sasa ni Jamal Malinzi, Rais anayetetea kiti chake, Iman Madega, Walles Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, Athumani Nyamlani na Shijja Richard.

Kwa upande wa nafasi ya makamu wa Rais wa TFF, ni mchuano kati ya Mulamu Ng’ambi, Mtemi Ramadhani, Michael Wambura na Geofrey Nyange (Kaburu).

“Nagombea nafasi urais wa TFF, wachezaji wa zamani na wadau wengine wa mpira wa miguu watatusindikiza mimi pamoja na mwenzangu Mtemi Ramadhani ambaye atagombea umakamu wa Rais,” amesema Ally Mayai.

error: Content is protected !!