Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Heche atema cheche Dodoma
Habari za Siasa

Heche atema cheche Dodoma

Spread the love

JOHN Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), amesema haogopi kuunganishwa katika kesi ya wananchi wa Tarime waliovamia mgodi wa North Mara kufuatia tamko alilolitoa wiki iliyopita ndani ya Bunge, anaandika Dany Tibason.

Wiki iliyopita, Heche alisema atawaongoza wananchi wa jimbo lake kuvamia katika mgodi wa Nyamongo, ili kuzuia uchimbaji wa madini unaofanywa na kampuni ya Acacia ambayo tayari serikali imetangaza kuwa ni kampuni ‘feki’ – isiyo na usajili.

Leo Jackline Msongozi, Mbunge wa Viti Maalum(CCM), amesema ni lazima Heche akamatwe na aunganishwe katika kesi ya waliovamia mgodi kwani yeye ndiye aliyewahamasisha wananchi hao.

Msongozi akichangia katika mjadala wa Bajeti ya serikali, amesema vurugu zinazoendelea Tarime zinatokana na mbunge wao kuwahamasisha kuvamia mgodi huo, hivyo ni muhimu jeshi la polisi likamkamata na kumuunganisha katika kesi hiyo,” amesema.

Heche alimpa taarifa mzungumzaji huyo akisema, “Napenda kumpa taarifa mchangiaji ambaye anaendelea kuchangia kuwa wananchi wa Tarime wamechukua hatua hizo baada ya kumuona Rais John Magufuli akihutubia na kusema anazuia wezi ambao wamekuwa wakitorosha madini.

“Kutokana na hali hiyo wananchi walichukua hatua ya kumuunga mkono Rais katika kuzuia wezi hao wa madini. Hata hivyo nataka kumwambia Mbunge anayezungumza kuwa mimi siogopi kuunganishwa na wananchi wangu, kama mnadhani nitaogopa basi niunganisheni nao.”

Awali Heche aliomba muongozo kutokana na matukio ambayo yanaendelea katika ngodi wa North Mara.
“Mhe. mwenyekiti kama ulivyosoma kwenye vyombo habari, jana na leo asubuhi, wananchi wa Tarime eneo la Nyamongo, wamemuunga mkono Rais vitendo, kwa kuingia kwenye mgodi wa North Mara kuzuia wizi ambao kamati zote za Rais zimethibitisha na kuwatangazia wananchi.

“Ni ajabu kwamba polisi wanatumia nguvu kubwa, kupiga wananchi na kuwaumiza, wakati wanatekeleza wito wa Rais kwamba tuungane kupambana katika vita hii ya kiuchumi. Mwqenyekiti naomba muongozo wako,” alisema Heche.

Akijibu muongozo uliombwa na Heche, mwenyekiti Zungu alimtaka Mbunge huyo kuonana na Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ili wapate njia muafaka ya kuweza kulitatua jambo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

Habari za Siasa

Dorothy Semu ajitosa kumrithi Zitto ACT-Wazalendo

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, anayemaliza muda wake, Dorothy...

error: Content is protected !!