Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge wadai bima ya maisha
Habari za SiasaTangulizi

Wabunge wadai bima ya maisha

Bunge likiendelea na vikao vyake
Spread the love

WABUNGE wameshangazwa kitendo cha ofisi ya bunge kupitia Jumuiya ya Madola (CPA) kushindwa kuwakatia bima ya maisha wabunge ambao wanamaliza muda wao kama umoha huo unavyotaka, anaandika Dany Tibason.

Mbunge wa Mwibala, Kangi Lugola (CCM) ndiye aliyekuwa wa kwanza kuibua mjadala huo bungeni wakati walipokuwa wakichangia muda mfupi baada ya wawasilisha mada kutoka CPA.

Naye Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) amesema wabunge wamegeuzwa kuwa sawa na ATM kwa kuwa imesengeka dhana kila mbunge anayo hela nyingi zaidi ya kusaidia jamii.

Mbali na hilo amesema wabunge wanashindwa kutimiza wajibu wao kutoka na wabunge kijifanya sehemu ya serikali badala ya kutambua kuwa wao wajibu wao ni kuisimamia serikali katika kufanya shuguli za maendeleo.

Naye Mbunge wa Same Mashariki, Nagenjwa Kaboyoka (Chadema) amesema anashangazwa kuona Tanzania ndiyo makao makuu ya Jumuiya ya Madola na Spika wa Tanzania ndiye rais.

Mbunge wa Songwe, Philipo Mlugo (CCM), amesema katika maelezo ya watoa mada walieleza katika Jumiya hiyo Waziri Mkuu ni Mlezi na Spika wa Bunge ni rais wa Jumuiya.

Kutokana na maelezo hayo Mulugo alitaka kujua nini majukumu ya Waziri Mkuu na nini majukumu ya spika kwani Jumiya ya Madola kwa Bunge la Tanzania ni kama limekufa.

Pia alitaka iwekwe bayana utofauti wa viwango vya malipo kati ya nchi ya Kenya na Tanzania kwani kunaonekana Bunge la Tanzania halitimizi majukumu yake ipasavyo licha ya kuwa wabunge wanakatwa kodi nyingi katika mishahara pamoja na magari.

Hata hivyo, Mulugo alihoji ni kwanini wabunge wanakatwa kiasi cha Sh. 1,200,000 kama kiinua mgogo cha mbunge na ni nani aliyetoa kibali hicho.

Akijibu hoja hizo, Said Yakubu, amesema ni haki ya mbunge lipata bima ya afya ya maisha kwani sheria zinaelekeza hivyo.

Aidha amesema kitendo cha wabunge wa Tanzania kugeuzwa kama ‘ATM’ ni mapenzi yao wenyewe kwani wabunge badala ya kuibana serikali na kushinikiza serikali ipeleke maendeleo imekuwa wakifanya wenyewe wabunge.

Katika semina hiyo ya wabunge ambayo lengo kuu lilikuwa kuwapatia elimu na maelekezo juu ya umuhimu wa mabunge ya jumuiya ya madola kazi zake na kuona kama utendaji wa wabunge hayo unaendana na utendaji wa Bunge la Tanzania.

Waliotoa semina hiyo ni Said Yakubu na Prof, David Mwamfupe. Katika semina hiyo, Yakubu alitoa mada juu ya muundo, shughuli na majukumu ya Jumuiya ya Madola.

Amesema Jumuiya ya Madola ni umoja wa hiari wa nchi 52 ambazo zilipata kuwa koloni la mwingereza isipokuwa nchi ya Rwanda na Msumbiji ambazo ziliomba kwa hiari kujiunga.

Yakubu amesema nchi hizo za jumuiya zinajumuisha nchi ambazo zina uchumi mkubwa, visiwa vidogo 30 vyenye idadi ya watu wasiozidi 100,000.

Amesema kuwa kitengo cha utafiti ya masuala ya Anuai yahusuyo bunge ulibaini masilahi mabalimbali ambayo utolewa kwa wabunge katika nchi mbalimbali.

Pia aliongeza kuwa katika nchi ya Kenya mbunge analipwa mshahara sawa na wa katibu mkuu wa Wizara, wanalipwa posho ya nyumba, mahudhurio, takrima ya nyumba na gharama za Jimbo.

Naye Prof Mwamfupe amesema malengo ya CPA katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Amesema ni malengo ya matamanio ya ulimwengu yanayokusudiwa kupeleka maendeleo ya kiuchumi, ujumuishwaji wa kijamii na endelevu wa mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

error: Content is protected !!