Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mapya yaibuka mauaji ya jambazi
Habari MchanganyikoTangulizi

Mapya yaibuka mauaji ya jambazi

Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Spread the love

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Taasisi za Kiislam Tanzania ameibuka na kumtetea anayeitwa jambazi aliyeuwawa katika tukio la uvamizi wa ATM, kuwa haukuwa jambazi, anaandika Hamisi Mguta.

Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuuwawa kwa Salum Mohammed Almasi, mmoja wa majambazi aliyekuwa akitekeleza uvamizi wa ATM nje ya jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini, Dar es Salaam.

Baada ya kutoa kwa tukio hilo na polisi kuthibitisha, Sheikh Ponda, amemuandika barua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kueleza utetezi wake juu ya kijana huyo aliyeuwawa.

Sheikh Ponda amechukua hatua hiyo baada ya kuzungumza na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na mtu huyo ambao wamedhihilisha kuwa Almasi hakuwa na vitendo viovu.

Sheikh Ponda ameuthibitishia mtandao huu kuwa ameandika barua hiyo kwa lengo la kutaka mazingatio katika mustakabali wa taifa.

Barua hiyo ya Sheikh Ponda ilieleza kuwa Mei 14, 2017, Almas alipigwa risasi na polisi hadharani kati ya majira ya saa 3:00-4:00 asubuhi wakati akitembea kwa miguu huko Kurasini.

“Nilipokea taarifa ya kijana Salum Muhamed Almasi aliyeuwawa hadharani kwa kupigwa risasi na polisi majira ya saa 3:00 na 4:00, asubuhi eneo la Kurasini Dar es Salaam akiwa anatembea barabarani kwa miguu.

“Kupitia taarifa ya polisi ni kuwa kijana huyo ni jambazi aliyetaka kupora fedha. Nimekutana na familia ya Marehemu ambaye ni mzaliwa wa Kilwa, familia inamtambua kuwa ni kijana mwema kabisa.

Nimeongea na baadhi ya wakazi wa Kilwa, wao pia wanamtambua kama mtu mwema kwa tabia na anayeshiriki ibada Msikitini ipasavyo,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

Aidha taarifa hiyo inasema Almasi pia alikuwa Imamu Msaidizi katika moja ya Misikiti huko Kurasini na muda mwingi ni mtu wa masomo.

“Amemaliza elimu ya msingi, kidato cha nne, cha tano, kidato cha sita na mpaka anauwawa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ngazi ya diploma fani ya ICT Network. Mh. Waziri mauwaji kama haya yanazidi kupambamoto Tanzania na yanachafua haiba ya Taifa,” imeeleza barua hiyo.

Hata hivyo wakati akitoa taarifa za ujambazi huo, Kamishna Sirro alinukuliwa akisema: “Inapotokea matukio kama haya wengi wamekuwa wakilinda nduguzao, hauwezi kujua ndugu yako amefanya nini hadi utakapobini ukweli wa jambo.”

Sheikh Ponda ameitaka serikali kutoa tamko la kufafanua mauaji yanayopoteza watu wengi kwa sasa pamoja na yanaendelea kutokea Kibiti, Pwani.

Amesema ikiwa mfumo wa nchi tuliourithi wa Mahakama, Bunge na Serikali una upungufu, basi busara ni kuuboresha na sio kuuhama na kuanzisha mwingine kinyemela.

2 Comments

  • Mimi na amini kabisa hilo eneo la bank linalindwa na cctv kamera. Basi uchunguzi uhusishe na ushahidi wa video kutoka cctv kamera.

  • Taarifa ya awali ilisema ndugu Salumu alikaidi agizo halali la kumtaka asimame ndio akipigwa na ya pili kutoka kwa kamanda Sirro inasema alijaribu kumnyang’anya askari bunduki ndio akafyatuliwa risasi kutoka nyuma.

    Sasa ipi ya kweli hapa. Mimi binafsi naweza nikasema ya kwanza inaukweli kwasababu Salum alikuwa na matatizo ya kusikia (alinikuta kidato cha sita 2009 Ndanda High School). Mwanahilisi naona ni vizuri mngelifanya uchunguzi binafsi wa hili tukio.

    Nb:Maelezo ya aya ya kwanza nimepata kutoka katika gazeti la mwananchi toleo la jumatatu na jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!