Friday , 24 May 2024
Home Kitengo Michezo Chelsea mabingwa England
MichezoTangulizi

Chelsea mabingwa England

Timu ya Chelsea ikishangilia ushindi
Spread the love

KLABU ya Chelsea ya jijini London, Uingereza, imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka England msimu wa 2016/17, baada ya kuifunga West Bromwich, bao 1-0 zilipochuana jana usiku, mabingwa hao wakiwa ugenini uwanja wa The Hawthorns, anaandika Jabir Idrissa.

Alikuwa mshambuliaji Michy Barshuayi, aliyeibeba kidedea Chelsea, alipopachika mpira wavuni dakika ya 82 kwa kiki baada ya kusogezewa mpira na Cesar Azpilicueta, aliyetumia makosa ya ngome ya West Brom kutofagia mpira ambao haukutarajiwa kuwa wa hatari.

Uimara wa ngome ya wenyeji ulivurugika baada ya kutolewa uwanjani beki Gareth McAuley.

Batshuayi, mara ya mwisho akiwa ameifungia Chelsea tarehe 20 Agosti mwaka jana, dhidi ya Watford, hajapata mafanikio ya ufungaji, lakini goli lake hilo bila shaka litaimarisha nafasi yake ya kuwa mchezaji anayeweza kusakwa na timu nyingine kwa ajili ya msimu ujao.

Chelsea iliyofikisha pointi 87 sasa kwa ushindi huo, ikiwa imebakiza mechi na Watford na Sunderland, kwenye uwanja wake wa Stamford Bridge, inafanikiwa kubeba ubingwa msimu huu chini ya kocha wake mpya Antonio Conte. Hakuna timu inayoweza kuzifikia alama hizo.

Huo utakuwa ni ubingwa wake wa sita tangu kombe hilo kuanzishwa. Haraka sherehe za ubingwa zililipuka jijini ikiwemo kwenye makao yake Stamford Bridge. Kwenye benchi la ufundi, goli la Batshuayi, aliyekuwa lawamani kwa kutochangamkia nyavu mara nyingi, liliwainua wenzake kwa shangwe kubwa ambako meneja Conte alikumbatia wachezaji kama ishara ya kuanza kwa furaha isiyo na kifani.

Conte ni kocha wa nne kwa Wataliano waliobeba ubingwa nchini Uingereza, akitanguliwa na Carlo Ancelotti (2009/10), Roberto Mancini (2008) na Claudio Ranieri (2000/04).

Ni mpuuzi gani atakayeendeleza lawama dhidi ya Batshuayi kwa hilo? Chelsea imetangulia mapema kutwaa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu unaoingia wa 2017/18. Zinazofukuzia nafasi ni Tottenham, Liverpool Manchester City na Arsenal.

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Endelea kubashiri na Meridianbet, Ligi bado zipo

Spread the love BAADA ya ligi mbalimbali kutamatika, bado kuna ligi mbalimbali...

Habari za SiasaTangulizi

Watu 1,673 wamchangia Lissu Sh. 20 milioni kununua gari

Spread the loveWATU 1,673 wamechanga fedha zaidi ya Sh. 20 milioni kwa...

Habari MchanganyikoTangulizi

11 wafariki dunia baada ya mtambo wa Kiwanda cha Mtibwa Sugar kupasuka

Spread the loveWATU 11 wamefariki dunia huku watatu wakijeruhiwa katika ajali ya...

Habari za SiasaMichezo

Serikali yaanika mikakati maandalizi AFCON 2027

Spread the loveSerikali imesema inaendelea kufanya mazungumzo na wadau pamoja na wamiliki...

error: Content is protected !!