Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli amtaka Ney wa Mitego aboreshe ‘Wapo’
Habari za SiasaMichezoTangulizi

Rais Magufuli amtaka Ney wa Mitego aboreshe ‘Wapo’

John Magufuli, Rais wa Tanzania
Spread the love

JOHN Magufuli, Rais wa Tanzania, ameliagiza Jeshi la Polisi kumwachia huru msanii wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ huku akimshauri kuporesha wimbo wake wa Wapo, anaandika Faki Sosi.

Ney wa Mitego alikamatwa na polisi mkoani Morogoro juzi usiku na kuleta jijini Dar es Salaam kwa madai ya kuimba wimbo uliokuwa na maneno yanayoikashifu serikali na viongozi wake.

Rais Magufuli kupitia kwa Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, Michezo, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Rais Magufuli amevutiwa na wimbo huo kutokana na kueleza hali halisi na kwamba ameshauri kuwa wimbo huo ungeendelezwa klwa kuwataja wakwepa kodi, wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya, na watu wanaofanya mambo yasiyofaa katika jamii.

Dk. Mwakyembe alidai kuwa Rais alimuambia kuwa: “Huyo kijana wako (Ney) aboreshe huo wimbo asiondoe chochote ila angoze aileze changamoto za jamii halafu aitike kama ulivyo wimbo wenye ‘wapo’… wauza madawa ya kulevya wapo… wakwepa kodi wapo…” alidai Dk Mwakyembe .

Dk  Mwakyembe alikiri kuwa alishauriwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kuhusu wimbo huo na kwamba aliwaambia wauwachie.

Baadhi ya mashairi yaliyokuwepo kwenye wimbo huo , “Hivi Uhuru wa Kuongea bado upo? Siamini nchi inaendeshwa kwa kiki! Nasikia kuna viongozi wamefoji vyeti? Wapooo! Mheshimiwa hivi unamjua Bashite kutoka Kolomije? We si Dokta wa kutumbua majipu?”

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!