August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mashabiki wa soka wamliza Nape

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (Kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe wakitazama mechi kati ya Taifa Stars na Botswana

Spread the love

UPENDO ambao mashabiki wa mpira wa miguu waliuonesha jana kwa Nape Nnauye, aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo ulimliza kiongozi huyo, anaandika Charles William.

Mashabiki wa soka waliojitokeza Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa – Taifa Stars dhidi ya Botswana, walisimama kwa muda na kumshangilia Nape Nnauye alipoingia uwanjani hapo, ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono.

Katika ukurasa wake wa Instagram leo, Nape ameweka video inayonesha mashabiki wakimshangilia kama ishara ya kumtia moyo, huku akiandika “Jana mlinitoa machozi.”

Nape ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi aliondolewa katika nafasi yake Alhamis ya wiki hii na Rais John Magufuli, ikiwa ni siku moja tu baada ya kueleza kuchukizwa na kitendo cha uvamizi wa ofisi za kituo cha Clouds TV, uliongozwa na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Siku hiyohiyo pia Nape alikabiliwa na maofisa usalama, ili kuzuiwa kuzungumza na wanahabari baada ya kuenguliwa katika wadhifa wake. Tukio la kumzuia Nape liliambatana na mmoja wa maofisa usalama kumnyoshea bastola ili kumshinikiza aingie kwenye gari lake na asizungumze na wanahabari.

Tangu kutokea kwa tukio hilo watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, wasanii, wananchi na wasomi wamejitokeza na kulaani kitendo alichofanyiwa Nape, huku wakimtia moyo.

Wamekuwa wakimtaka aendelee kusimamia haki pasipo kuyumba wala kuogopa.

error: Content is protected !!