Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mauaji ndani ya msikiti Canada
Habari MchanganyikoKimataifa

Mauaji ndani ya msikiti Canada

Spread the love

WAUMINI sita wa Dini ya Kiislam nchini Canada, wamefariki dunia na wanane kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi katika msikiti wa Quebec usiku wa kuamkia leo, anaandika Hamis Mguta.

Watu wawili walivamia kwenye msikiti huo na kuanza kuwamiminia risasi waumini wa dini hiyo walikokuwa kwenye Swala ya Isha katika msikiti huo.

Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada ameita tukio hilo ‘shambulio la kigaidi’ ambapo polisi wa mji huo wameeleza kuwa, watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika kwenye shambulio hilo wamekamatwa.

Mohamed Yangui, imami wa msikiti huo ambaye hakuwepo wakati wa shambulio hilo ameeleza kupokea taarifa kuwa,  watu watano walifariki dunia papo hapo.

Hata hivyo, mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo ameeleza kuwa, aliwaona wanaume watatu wakiwa na silaha wakishambulia watu zaidi ya 40 ndani ya msikiti huo.

“Watu sita wamefariki dunia, umri wao ni kati ya miaka 35 na 70,” imeeleza taarifa ya Christine Coulombe, Mkuu wa Polisi katika Jimbo la Quebec na kuongeza watu wanane wamejeruhiwa.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo ameeleza kulaani tukio hilo “tunalaani tukio hilo la mauaji ya kigaidi ndani ya msikiti tena watu wakiwa wanafanya ibada” amesema na kuongeza;

“Jamii ya Waislam ni sehemu ya watu muhimu ndani ya taifa hili. Fikra za kipuuzi na kuhusisha Uislam na ugaidi hazina nafasi kwenye miji, wilaya na taifa hili.”

Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki wakati ambao serikali ya nchi hiyo imeeleza kuwa tayari kupokea watu wanaofukuzwa na Serikali ya Donald Trump nchini Marekani.

Serikali ya Canada imeeleza kuwa, ipo tayari kupokea watu wote wanaofukuza nchini Marekani na kuwahudumia bila kujali imani za dini zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!