Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif amfungulia mlango Dk. Shein
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif amfungulia mlango Dk. Shein

Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar (kushoto) walipokuwa katika mazungumzo ya muafaka na Maalim Seif Shariff Hamad
Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) amempa nafasi tena Dk. Ali Mohamed Shein ili kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza katika kipindi cha televisheni ya Azam, kinachoongozwa na mwanahabari mkongwe Tido Mhando, Maalim amesema CUF haitambui marudio ya uchaguzi mkuu Zanzibar yaliyofanyika Machi 2016 kama ambavyo CCM haitambui ushindi wake wa Oktoba 2015.

Itakumbukwa kuwa mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ulijitokeza baada ya Jecha Salim Jecha mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 wa mwaka 2015 ambayo CUF na Maalim Seif wanaamini walishinda.

“Hata kulipokuwa na Seriali ya Umoja wa Kitaifa mambo yalikuwa mazuri, kulikuwa na maelewano na mtu akifika ofisini anashindwa kufahamu CUF ni nani na CCM ni nani,” amesema Maalim Seif.

Maalim Seif amesisitiza kuwa alishinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa terehe 25 Oktoba, 2015 uliofutwa na kwamba alistahili kutangazwa kuwa Rais wa Zanzibar.

“Jecha na CCM wawaeleze Watanzania uchaguzi wa mwaka 2015 ulifutwa kwa kutumia Ibara gani ya Katiba ya Zanzibar au Kifungu kipi cha sheria? Kwasababu hakuna sehemu yoyote katika Katiba au Sheria za Zanzibar ambapo Tume ya Uchaguzi au mwenyekiti wake anapewa mamlaka ya kufuta uchaguzi.

Uchaguzi ulifutwa bila kufuata sheria wala Katiba na hivyo hata marudio yake yalikuwa haramu ndiyo maana hatukushiriki,” amesema Maalim.

Kuhusu mgogoro unapendelea ndani ya chama hicho amesema ni wa “kupandikizwa na serikali ya CCM kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa na vyombo vya dola.”

Amemtupia lawama Jaji Francis Mutungi kwa kuidhinisha malipo ya Sh. 360 milioni ambayo ni sehemu ya ruzuku ya chama hicho kwenda mikononi mwa Prof. Ibrahim Lipumba na kundi lake bila Bodi ya Wadhamini ya CUF kujua wala yeye ambaye ni Katibu Mkuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!