Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Uganda kuivaa Ghana leo AFCON
Michezo

Uganda kuivaa Ghana leo AFCON

Kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda 'The Crances'
Spread the love

TIMU ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ leo itatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) inayofanyika nchini Gabon dhidi ya timu ya taifa ya Ghana ‘The Black Stars’ kwenye mchezo wa kundi D.

Uganda ndio timu pekee iliyofanikiwa kufuzu michuano hiyo kutokea ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, ambao ulikuwa hauna mwakilishi katika michuano hiyo katika kipindi cha muda mrefu kutokana na timu zake kutofanya vizuri katika michezo ya kufuzu.

Mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na ubora wa wachezaji na vikosi walivyokuwa navyo, Ghana inafahamika ni timu ngumu na yenye uzoefu katikia michuano hiyo kwa miaka ya hivi karibuni kutokana kuwa na wimbi kubwa la wachezaji wanaocheza katika ligi kubwa barani Ulaya.

Mechi nyingine itakayopigwa katika kundi hilo leo, itazikutanisha timu za Mali dhidi ya Misri majira ya saa nne usiku, na itatoa msimamo kamili wa kundi hilo ambalo linaonekana kuwa gumu kutokana na ubora wa timu zilizopo humo.

Uganda ambayo kwa sasa inafuzu michuano hiyo kwa mara ya pili, toka mwaka 1978, imekuwa na mafanikio makubwa kwenye soka kwa siku za hivi karibuni kiasi cha kushinda tuzo ya timu bora ya CAF katika hafla iliyofanyika Nigeria, huku mlinda mlango wao namba moja Denis Onyango akitwaa tuzo ya mchezaji bora kwa wanaocheza ligi ya ndani Afrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

error: Content is protected !!